Lugha Nyingine
Mawaziri wa Afrika wapitisha maamuzi ya kuhimiza maendeleo ya kidijitali, maendeleo ya kiuchumi
Mawaziri wa Afrika wanaosimamia mawasiliano na teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) wamepitisha maamuzi mapya yenye lengo la kuharakisha mageuzi ya kidijitali barani Afrika, kuinua maendeleo ya kijamii na kiuchumi, kuongeza nafasi za ajira na kuboresha maisha ya watu katika bara zima.
Uamuzi huo umepitishwa Jumanne kwenye ufungaji wa mkutano wa tano wa Kamati Maalumu ya Kiufundi (STC) kuhusu TEHAMA barani Afrika.
Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Afrika (AU), imesema mawaziri hao wameeleza dhamira ya kuongeza uhusiano kati ya mfumo wa kidijitali, mabadiliko ya tabianchi, miundombinu na nishati ili kuongeza manufaa ya suluhisho za kidijitali.
Mawaziri hao pia wameahidi kupigania kupitishwa kwa Mkakati wa Mageuzi ya Kidijitali kwa Afrika na Mpango wa Utekelezaji wake, kama sehemu ya mradi mkuu wa Ajenda ya Umoja wa Afrika ya 2063 kwenye Mkutano wa wakuu wa Umoja wa Afrika utakaofanyika mwaka 2024.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma