Lugha Nyingine
Bandari kavu ya Erenhot nchini?China yashughulikia safari zaidi ya 3,000 za treni za mizigo za kati ya China na Ulaya
Treni ya mizigo inayotoa huduma kati ya China na Ulaya ikipita kwenye lango la taifa katika Bandari ya Erenhot iliyoko Mkoa wa Mongolia ya Ndani, Kaskazini mwa China, Januari 8, 2021. (Picha na Guo Pengjie/Xinhua) |
HOHHOT - Bandari ya Erenhot iliyoko katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, Kaskazini mwa China imeshughulikia safari zaidi ya 3,000 za treni za mizigo zinazotoa huduma kati ya China na Ulaya hadi kufikia sasa mwaka huu, mamlaka ya reli ya China imesema siku ya Jumanne.
Hii ni ni mara ya kwanza kwa bandari hiyo ya reli kurekodi idadi kubwa kama hiyo ya treni za mizigo kati ya China na Ulaya ndani ya mwaka mmoja tangu huduma yake ya treni za mizigo za kati ya China na Ulaya kuzinduliwa Mwaka 2013.
Bandari ya Erenhot ni bandari kavu kubwa zaidi kati ya China na Mongolia. Imekuwa ikitoa urahisi kwa treni za mizigo kati ya China na Ulaya tangu mwanzoni mwa mwaka huu, ikiboresha ufanisi wa uendeshaji wa huduma hiyo.
Jumla ya safari za treni za mizigo kati ya China na Ulaya kupitia bandari hiyo kati ya Mwaka 2013 na nusu ya pili ya Mwaka 2019 ilifikia takriban 3,000. Hata hivyo, idadi hiyo hiyo kwa sasa imefikiwa ndani ya mwaka mmoja, ikithibitisha ukuaji mkubwa wa usafirishaji wa mizigo wa bandari hiyo, kwa mujibu serikali za mitaa katika mkoa huo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma