Lugha Nyingine
China yakataa madai ya EU juu ya kuuza nje magari ya umeme (EV) yaliyozalishwa kuliko mahitaji halisi ya soko
Picha hii iliyopigwa Novemba 15, 2023 ikionyesha sehemu ya jengo la Kamisheni ya Ulaya huko Brussels, Ubelgiji. (Xinhua/Zhao Dingzhe)
BRUSSELS - Balozi wa China katika Umoja wa Ulaya (EU) Fu Cong amekataa madai ya hivi majuzi kwamba China inauza kupita kiasi kwenye soko la Ulaya magari yanayotumia umeme (EV) yaliyozalishwa kwa wingi kuliko mahitaji halisi ya soko.
"Nataka kusisitiza jambo kwamba kwakuwa tu kampuni ya China zinauza magari barani Ulaya haimaanishi kuwa na uzalishaji mwingi wa magari kuliko mahitaji halisi ya soko," balozi huyo amesema kwenye mkutano wa Baraza la Ulaya na China uliofanyika Brussels na kuandaliwa na Marafiki wa Ulaya, shirika lisilo la faida kwa ajili ya sera ya EU lenye makao yake makuu mjini Brussels.
Washiriki wapatao 300, wakiwemo watunga sera, wafanyabiashara na watafiti, walihudhuria mkutano wa baraza hilo.
Picha hii iliyopigwa Septemba 4, 2023 ikionyesha gari aina ya Seal linalotumia umeme la Kampuni ya BYD kwenye hafla ya kuonesha bidhaa kwa waandishi wa habari ya Maonyesho ya Kimataifa ya Magari (IAA) Mwaka 2023 mjini Munich, Ujerumani. (Xinhua/Zhang Fan)
Hoja juu ya kuzalisha kwa wingi magari ya umeme kuliko mahitaji ya soko iliibuliwa na Umoja wa Ulaya wakati unajiandaa kwa mkutano wa kilele wa pande mbili na China, ulioripotiwa kupangwa kufanyika mwezi ujao.
Wiki iliyopita, Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen alisisitiza, "Ni wazi kuna uzalishaji mwingi wa magari ya umeme kuliko mahitaji ya soko nchini China, na magari haya yaliyozalishwa kwa wingi kuliko mahitaji halisi yatasafirishwa nje," akidai hii ndiyo sababu ya EU kuanzisha uchunguzi wa kupinga China kutoa ruzuku kwa kampuni zinazozalisha magari ya umeme (EV).
Akitupilia mbali madai hayo, Fu ameuliza swali: "Ikiwa kutafuta soko la ng'ambo kunaweza kufasiriwa moja kwa moja kama kuzalisha kwa wingi kuliko mahitaji halisi, basi kampuni za Ulaya zinafanya nini katika soko la China?"
Ameelezea wasiwasi wake kama haki kweli itatendeka katika uchunguzi huo ulioanzishwa na EU na taratibu zake, akielezea matumaini kwamba "busara inaweza kutawala" wakati wa majadiliano juu ya suala hilo.
Picha hii iliyopigwa Septemba 4, 2023 ikionyesha gari aina ya Seal linalotumia umeme la Kampuni ya BYD kwenye hafla ya kuonesha bidhaa kwa waandishi wa habari ya Maonyesho ya Kimataifa ya Magari (IAA) Mwaka 2023 mjini Munich, Ujerumani. (Xinhua/Zhang Fan)
Balozi Fu ameihakikishia sekta ya biashara kwamba China imejitolea kufanya mageuzi na kufungua mlango, na kuhimiza maendeleo yenye ubora wa juu. "Hii ina maana fursa zaidi kwa kampuni za Ulaya."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma