Lugha Nyingine
Rais Mwinyi wa Zanzibar aalika wawekezaji katika sekta za viwanda na biashara kutoka China
Rais wa Tanzania Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amewakaribisha Zanzibar wafanyabiashara wakubwa na wenye viwanda kutoka China kuwekeza katika sekta mbalimbali visiwani Zanzibar.
Rais Mwinyi amewakaribishwa wawekezaji hao kwenye mazungumzo yaliyofanyika Novemba 21, Ikulu mjini Unguja alipokuwa akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Wafanyabiashara Wenye Viwanda la China, Bw. Xu Lejiang na wafanyabiashara 15 kutoka China. Amewaelezea kuwa utalii hasa wa hoteli na maeneo ya kupumzikia una fursa nyingi za uwekezaji, kwani Zanzibar ina maeneo mazuri ya fukwe nyeupe zinazowavutia wageni na watalii wengi.
Bw. Xu Lejiang amemwelezea Dk Mwinyi kwamba shirikisho hilo limeziweka pamoja kampuni kubwa na viwanda zaidi ya 700 wakiwemo wafanyabiashara wa madini, kampuni za vifaa vya ujenzi, teknolojia na kilimo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma