Lugha Nyingine
Mkutano wa masoko ya hisa ya Afrika kuongeza biashara ya kuvuka mipaka kwa mitaji ya masoko
Wawakilishi wa masoko ya hisa barani Afrika wamekutana katika mkutano wa siku mbili ulioanza Alhamisi jijini Nairobi, Kenya, kwa lengo la kuongeza biashara ya kuvuka mipaka kwa kampuni zilizoorodheshwa kwenye masoko ya hisa na dhamana.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 26 wa Mwaka wa Shirikisho la Masoko ya Dhamana na Hisa la Afrika (ASEA), Rais wa Kenya William Ruto amesema biashara ya soko la hisa na dhamana za kampuni zilizoorodheshwa kati ya nchi za Afrika itawezesha kuongeza idadi kubwa ya wawekezaji katika soko la mitaji barani humo, na kuongeza kuwa, biashara hiyo pia itawezesha nchi mbalimbali kujifunza njia bora za utenda kazi ndani ya mfumo mmoja wa kiuchumi.
Katika mkutano huo, washiriki watatafuta suluhisho thabiti la changamoto zinazoikabili sekta hiyo, na kuwezesha kuwa na mfumo wa kiuchumi wa soko la fedha la Afrika ambalo ni jumuishi na imara.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma