Lugha Nyingine
Mjasiriamali wa Nigeria aiishi ndoto yake mkoani Hainan, China
Joy Nkiru Ikpeoha, ambaye ni mjasiriamali kutoka Nigeria akitambulisha kampuni na huduma zake kwa raia wa kigeni wanaoishi Haikou, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China Mei 19, 2023. (Xinhua)
Ni mafanikio gani mtu anaweza kuyafikia ndani ya miaka minane? Joy Nkiru Ikpeoha kutoka Nigeria amepata shahada yake ya kwanza na ya uzamili na kuanzisha kampuni yake ndani ya muda huo.
Ikpeoha, aliyezaliwa mwaka 1992, alifika kwa mara ya kwanza kwenye mkoa huo wa kisiwa wa Hainan kusini mwa China Mwaka 2015, ili kujifunza lugha ya Kichina katika Chuo Kikuu cha Hainan. Miaka minne baadaye, aliendeleza utafutaji wake wa elimu, na mwishowe alipata shahada ya uzamili ya usimamizi wa biashara Mwaka 2022.
Safari ya kijasiriamali ya Ikpeoha ilianza mwaka huu wakati alipoanzisha kampuni katika mji mkuu wa mkoa huo Haikou, ikiwa na lengo la kutoa jukwaa la huduma kwa haraka na ufanisi kwa vipaji vya aina zote vya raia wa kigeni.
“Kampuni yangu inahusika na kusaidia vipaji vya raia wa kigeni wanaoishi Haikou au sehemu nyingine za Hainan kuanzisha biashara zao wenyewe, na kuwafanya wahisi wako nyumbani hapa Hainan,” Ikpeoha ameeleza. Kampuni hiyo pia inatoa huduma nyingine kwa raia wa kigeni, ikiwemo ukalimani na usaidizi wa kutafuta nyumba za kupanga.
Ikpeoha anaona amebarikiwa kwamba ameweza kuanzisha biashara yake mwenyewe kutoka hatua za mwanzo, kutokana na msaada wa sera ya Bandari ya Biashara Huria ya Hainan. “Mazingira haya yanafaa kabisa kwa wajasirimali vijana, hasa kwa raia wa kigeni wasio na pesa nyingi kuanzisha kampuni zao.”
Akiwa alikuwa na ndoto ya kuwa na kampuni yake mwenyewe tangu alipoanza kusomea shahada ya usimamizi wa biashara, sasa Ikpeoha anafurahi sana kuwa “ndoto yake imetimizwa.”
Joy Nkiru Ikpeoha, mjasiriamali kutoka Nigeria, akifanya kazi kwa kompyuta kwenye ofisi yake huko Haikou, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China tarehe 15, Novemba 2023. (Xinhua/Guo Cheng)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma