Lugha Nyingine
Rais wa China awasili San Francisco, Marekani
(CRI Online) Novemba 15, 2023
(Picha inatoka CRI.)
Rais Xi Jinping wa China amewasili mjini San Francisco, Marekani jana mchana kwa saa za huko, ambako atakutana na rais wa Marekani Joe Biden, na pia atahudhuria Mkutano wa 30 wa Kilele wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki (APEC) kuanzia tarehe 14 hadi 17.
Rais Xi alipokelewa na viongozi wa ngazi ya juu wa Marekani katika Uwanja wa Ndege wa San Fransisco, akiwemo mkuu wa Jimbo la California Gavin Newsom, Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen.
Wamarekani wenye asili ya China na wanaoishi au kusoma nchini Marekani, walijipanga kando ya barabara aliyopita Rais Xi wakipeperusha bendera za China na Marekani kukaribisha kwa furaha ziara ya Rais Xi Jinping.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma