Lugha Nyingine
Afrika yashuhudia ukuaji endelevu wa mifumo ya malipo ya papo hapo
Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika (UNECA), imesema Afrika inashuhudia ukuaji endelevu na mahitaji ya mifumo ya malipo ya papo hapo.
Toleo la pili la ripoti ya kila mwaka ya mfumo jumuishi wa malipo ya papo hapo (SIIPS) barani Afrika, inasema mafanikio hayo yanaonyesha maendeleo madhubuti ya Afrika kuelekea lengo linalotarajiwa la kuwa na mifumo ya malipo ya papo hapo ya pande zote na shirikishi, kama sehemu ya Miundombinu ya Kidijitali ya Umma ya Afrika (DPI), inayounda mfumo ikolojia wa kidijitali kwa watu, biashara na serikali.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mifumo mitatu mipya ya malipo ya papo hapo ambayo imezinduliwa nchini Ethiopia, Morocco na Afrika Kusini katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, na kufanya jumla ya mifumo ya papo hapo ya ndani ya nchi na ya kikanda katika Bara la Afrika kufikia 32.
Ripoti pia imesema mifumo hiyo imewezesha miamala karibu bilioni 32 yenye thamani ya dola takriban trilioni 1.2 za Marekani kwa mwaka 2022.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma