久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

Maparachichi ya Kenya yapata soko lililo tayari la China baada ya kuoneshwa kwa mara ya kwanza katika CIIE

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 06, 2023

Kwenye shamba la parachichi lililopo kwenye Kaunti ya Nakuru, Kenya, Richard Wafula, mmiliki wa shamba hilo alikuwa na shughuli nyingi akivuna maparachichi pamoja na wafanyakazi wake.

“Punde takriban makontena 10 ya maparachichi mabichi yatawasilishwa kwa wateja wa China kutoka hapa,” alisema Wafula.

China na Kenya zilitia saini itifaki ya kuhimiza biashara ya pande mbili ya maparachichi mwezi wa Januari, 2022. Miezi saba baadaye, shehena ya kwanza ya maparachichi mabichi yaliyozalishwa Kenya iliingia kwenye soko la China, ikiifanya Kenya kuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuuza maparachichi mabichi China.

Mwezi Novemba, 2022, maparachcihi ya Kenya yalioneshwa kwa mara ya kwanza nchini China kwenye Maonyesho ya tano ya kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya nchi hiyo (CIIE), ambapo yalipendwa mara moja na wateja.

Picha ikionesha shamba la parachichi kwenye Kaunti ya Nakuru, Kenya. (Picha na Du Gongming)

Picha ikionesha shamba la parachichi kwenye Kaunti ya Nakuru, Kenya. (Picha na Du Gongming)

Richard Tuwei ni mkulima wa parachichi kutoka mji wa Magharibi mwa Kenya, Eldoret. Mwezi Agosti, 2022, bidhaa za shamba lake zilikuwa mojawapo ya maparachichi ya kwanza yaliyofaulu kigezo cha kuingia soko la China na kuuzwa kwa nchi hiyo.

“Hapo zamani wakati msimu wa mavuno ya parachichi ulipowadia, ilitubidi kungoja kwa muda kabla ya kuyachuma kwa sababu wafanyabiashara wenyeji walihitaji muda kutafuta wanunuzi. Lakini sasa tunachuma matunda mara tu baada ya kukomaa. Hitaji la soko la China ni kubwa sana, na bidhaa zetu zimepata kwa haraka soko lililo tayari. Fursa hii mpya imetuhamasisha kupanda miti 500 mingine ya parachichi mwaka jana,” Tuwei ameliambia gazeti la People’s Daily.

“China ina idadi kubwa ya watu, ambayo ni mali muhimu kwa soko lolote. Tunaamini kuwa siku za baadaye, wakulima wengi zaidi watauza maparachichi China,” amesema Kello Harsama, Katibu Mkuu katika Idara ya Taifa anayeshughulikia maendeleo ya mazao ya kilimo katika Wizara ya Maendeleo ya Kilimo na Mifugo ya Kenya.

Mbia wa Wafula na Tuwei ni kampuni ya China ya Greenchain yenye makao yake makuu mjini Shanghai. Mwezi wa Agosti mwaka jana, shehena ya kwanza ya maparachichi kutoka Kenya ilifika China katika makontena manne. Mwaka huu, kampuni ya Greenchain tayari imesha safirisha makontena 100 ya maparachichi nchini China, na namba hiyo inakadiriwa kuja kufikia 300 katika mwisho wa mwaka huu.

“Maonyesho ya CIIE yameleta athari dhahiri za kuongeza mauzo, kuhimiza hali ya manufaa ya pande zote kwa wahusika wanaoshiriki,” amesema Du Gongming, meneja mkuu wa kampuni ya Greenchain anayeshughulikia biashara ya Afrika.

Maparachichi yakipakiwa kwenye lori kwenye kiwanda cha kusindika maparachichi cha Kampuni ya Greenchain. (Picha na Chen Yongjian)

Maparachichi yakipakiwa kwenye lori kwenye kiwanda cha kusindika maparachichi cha Kampuni ya Greenchain. (Picha na Chen Yongjian)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>