Lugha Nyingine
Kampuni zaidi ya 15 za Zimbabwe kushiriki maonyesho ya uagizaji bidhaa ya China
HARARE - Kampuni zaidi ya 15 za Zimbabwe zitashiriki katika Maonyesho ya 6 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) yatakayofanyika Shanghai kuanzia Novemba 5 hadi 10, huku shirika la maendeleo na uhamasishaji biashara la nchi hiyo, ZimTrade likitarajia kuona biashara ikiimarika kati ya nchi hizo mbili.
ZimTrade itawaongoza wadau kwenye maonyesho hayo kwa lengo la kubainisha na kuzalisha fursa za kibiashara kwa kampuni za Zimbabwe.
Kampuni zitakazoshiriki katika maonyesho hayo zimetolewa kutoka sekta ya ngozi, vyakula vilivyosindikwa, sanaa na ufundi, mawasiliano ya simu, madini, nishati na utalii, ZimTrade imesema siku ya Jumatatu.
Shirika hilo limesema uhusiano kati ya China na Zimbabwe umekuwa ukiimarika huku China ikiwa nchi ya tatu duniani kwa kuingiza bidhaa za Zimbabawe katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
“Mtazamo umekuwa katika kuongeza biashara kati ya nchi hizo mbili, kutumia fursa muhimu katika biashara,” imesema ZimTrade. Zimbabwe na China Mwaka 2022 zilitia saini itifaki ya machungwa, "ambayo tangu wakati huo imeshuhudia mazao ya matunda jamii ya machungwa, ambayo yanahitajika sana nchini China, yakisafirishwa nchini humo."
"Mapema mwaka huu kampuni za Zimbabwe pia zilikwenda Beijing kushiriki kwenye Jukwaa la Biashara kati ya China na Zimbabwe kutafuta fursa za kuuza bidhaa nje na kuelewa vyema soko la China," shirika hilo la biashara limesema.
Limeongeza kuwa Kongamano la Biashara kati ya China na Zimbabwe ni msingi mzuri wa kuendeleza uelewa wa soko na bidhaa zinazohitajika ambazo Zimbabwe inaweza kutoa.
Takwimu za shirika hilo zinaonesha kuwa Mwaka 2022 China iliagiza bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 1.3 kutoka Zimbabwe, huku Zimbabwe ikiagiza bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 1.13 kutoka China, hivyo kudhihirisha uwiano wa kibiashara wenye manufaa kati ya nchi hizo mbili.
Habari ya picha ya wanandoa wapanda msitu katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
Mandhari ya majira ya Mpukutiko katika Kaunti ya Gongbo'Gyamda mjini Nyingchi, Mkoa wa Tibet, China
Tamasha la 15 la Mitindo ya Mavazi na Uanamitindo la Afrika lafanyika nchini Benin
Mandhari ya Hifadhi ya Taifa ya Mazingira Asilia ya Milima ya Altun katika Mkoa wa Xinjiang, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma