Lugha Nyingine
Mkutano wa Baraza la Boao la China kufuatilia zaidi maendeleo na usalama wa dunia
Picha hii iliyopigwa kutoka angani Juni 8, 2023 ikionyesha mandhari ya eneo lenye mandhari nzuri la Kisiwa cha Chungwa huko Changsha, Mkoa wa Hunan, Katikati mwa China. (Xinhua/Chen Sihan)
CHANGSHA - Mkutano wa pili wa Jukwaa la Maendeleo ya Kiuchumi na Usalama wa Dunia la Baraza la Boao la Asia (BFA) umefunguliwa huko Changsha, mji mkuu wa Mkoa wa Hunan katikati mwa China siku ya Jumapili.
Ukiwa na kaulimbiu isemayo "Maendeleo ya Dunia, Usalama wa Pamoja," mkutano huo utafanyika kwa siku tatu.
Shughuli zaidi ya 30, ikiwa ni pamoja na hafla ya ufunguzi, majukwaa madogo, majadiliano ya wanajopo na maonyesho zimepangwa kufanyika. Maofisa wa serikali, wakuu wa mashirika ya kimataifa, wajumbe wa wafanyabiashara na wasomi watakusanyika ili kuchangia maoni yao kuhusu masuala yanayofuatiliwa zaidi katika maendeleo na usalama wa Dunia, kama vile usalama wa chakula, usalama wa mambo ya fedha na usalama wa nishati.
Mkutano huo umeandaliwa kwa pamoja na Baraza la Boao la Asia (BFA) na serikali ya Mkoa wa Hunan. Mkutano wa kwanza wa Jukwaa la Maendeleo ya Kiuchumi na Usalama wa Dunia la Baraza la Boao la Asia ulifanyika Changsha, China Mwaka 2021.
Mandhari ya Hifadhi ya Taifa ya Mazingira Asilia ya Milima ya Altun katika Mkoa wa Xinjiang, China
Kutalii Hifadhi ya Taifa ya Nairobi nchini Kenya kupitia lenzi ya kamera
Habari Picha: Watu wakitembelea Mlima Huashan katika Mkoa Shaanxi, Kaskazini Magharibi mwa China
Mandhari ya Ziwa Kanas katika Eneo la Altay, Mkoa wa Xinjiang, China wakati wa majira ya mpukutiko
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma