Lugha Nyingine
Mfanyabiashara wa Uganda asema China inatoa fursa za soko kwa kampuni za kigeni kupitia maonyesho ya uagizaji bidhaa
Fradan Tumukunde, afisa mauzo katika Kampuni ya Kahawa ya Star Cafe, akionyesha bidhaa za kahawa kutoka kwenye kampuni yake huko Mukono, katikati mwa Uganda, Oktoba 24, 2023. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)
MUKONO - China inatoa fursa kwa kampuni za kigeni kwa kuziruhusu kupata soko lake kubwa kupitia maonyesho mbalimbali kama vile Maonyesho ya Kimataifa ya Uagizaji na Uuzaji Nje wa Bidhaa ya China (CIIE), Fradan Tumukunde, mtaalamu wa kahawa kutoka Uganda, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua.
Tumukunde ni afisa mauzo wa Kampuni ya Kahawa ya Star Cafe. Katika Wilaya ya Mukono katikati ya Uganda, sehemu ya kukaanga na kufungasha katika kampuni ya kibinafsi imejaa harufu ya kuvutia ya kahawa wakati ambapo wafanyakazi wako katika pilika za kupakia kahawa kwa ajili ya soko la kimataifa, ikiwa ni pamoja na China.
Tumukunde anasema kampuni yake ina nia ya kufikia makubaliano ya kibiashara katika maonyesho hayo yajayo, na kwamba itakuwa ni mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kuonyesha bidhaa zake katika maonyesho hayo, ingawa bidhaa zao zimeonyeshwa katika maonyesho mengine nchini China.
Maonyesho ya 6 ya CIIE, yaliyopangwa kufanyika Novemba 5-10 mjini Shanghai, yanatarajiwa kuvutia mamia ya kampuni za kigeni zinazo nia ya kuingia soko la China.
Tumukunde ana matumaini kuwa katika maonyesho hayo, atawasiliana na vijana zaidi wa China ambao wako tayari kujaribu bidhaa za kahawa kutoka Uganda.
Kuna kizazi cha vijana nchini China ambao "wako tayari kufuatilia na kununua kahawa zaidi. Hili ndilo linaloongoza manunuzi ya juu ya matumizi ya kahawa nchini China," amesema.
Amesema kwa mujibu wa utafiti wa kampuni yake, soko la China limekuwa likipanuka, na hilo litachochea shauku ya wafanyabiashara wadogo na wa kati (SMEs) nchini Uganda na barani Afrika.
"Maonyesho haya yako wazi, yanatukutanisha wanunuzi wahitaji na ninaamini kampuni ndogo na ya kati ya Uganda au Afrika inaweza kuja na kutafuta soko hili," ameongeza.
Picha hii iliyopigwa Oktoba 24, 2023 ikionyesha bidhaa za kahawa kutoka Kampuni ya Kahawa ya Star Cafe huko Mukono, katikati mwa Uganda, Oktoba 24, 2023. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)
Mandhari ya Hifadhi ya Taifa ya Mazingira Asilia ya Milima ya Altun katika Mkoa wa Xinjiang, China
Kutalii Hifadhi ya Taifa ya Nairobi nchini Kenya kupitia lenzi ya kamera
Habari Picha: Watu wakitembelea Mlima Huashan katika Mkoa Shaanxi, Kaskazini Magharibi mwa China
Mandhari ya Ziwa Kanas katika Eneo la Altay, Mkoa wa Xinjiang, China wakati wa majira ya mpukutiko
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma