Lugha Nyingine
Uchumi wa China kudumisha kasi ya kuimarika: Mwanauchumi wa J.P. Morgan
Picha hii ya iliyopigwa Januari 10, 2023 inaonyesha mandhari ya eneo la Lujiazui katika Eneo la Majaribio la Biashara Huria la China (Shanghai) lililoko Shanghai, Mashariki mwa China. (Xinhua/Fang Zhe) |
BEIJING - Uchumi wa China utadumisha kasi nzuri ya kuimarika katika robo ya nne ya mwaka 2023 wakati ambapo takwimu za uchumi za robo tatu za mwaka huu zimezidi makadirio ya awali, kwa mujibu Zhu Haibin, mchumi mkuu katika taasisi ya kifedha ya J.P. Morgan, Tawi la China.
Katika mahojiano na Shirika la Habari la China, Xinhua hivi karibuni, mchumi huyo amesema muda mfupi baada ya China kutoa takwimu za kiuchumi za robo tatu za kwanza za mwaka huu, J.P. Morgan ilirekebisha kwa kuinua makadirio yake ya ukuaji wa pato la taifa la China (GDP) Mwaka 2023 kutoka asilimia 5 hadi asilimia 5.2.
"Pato la Taifa la China katika robo tatu linazidi makadirio. Kufuatia takwimu bora za uchumi kuliko ilivyotarajiwa mwezi Agosti, ufanisi wa uchumi wa Mwezi Septemba tena umezidi makadirio yetu, kwani viashiria vikuu kama vile uzalishaji viwandani, mauzo ya rejareja na mauzo ya nje yalikuwa mazuri zaidi," Zhu alisema kuhusu kupanda kwa makadirio hayo.
"Ukuaji uliokadiriwa wa asilimia 5.2 ni kiwango bora cha ukuaji kote duniani," amesema.
Uchumi wa China uliongezeka kwa asilimia 4.9 mwaka hadi mwaka katika robo ya tatu ikilinganishwa na robo ya tatu ya mwaka jana. Katika robo tatu za kwanza za Mwaka 2023, uchumi ulikua kwa asilimia 5.2, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Idara ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) mapema mwezi huu.
Maofisa wa serikali ya China wamesema ukuaji huu wa uchumi unaweka msingi thabiti wa kufikia lengo la taifa la ukuaji wa asilimia 5 kwa Mwaka 2023.
Mandhari ya Hifadhi ya Taifa ya Mazingira Asilia ya Milima ya Altun katika Mkoa wa Xinjiang, China
Kutalii Hifadhi ya Taifa ya Nairobi nchini Kenya kupitia lenzi ya kamera
Habari Picha: Watu wakitembelea Mlima Huashan katika Mkoa Shaanxi, Kaskazini Magharibi mwa China
Mandhari ya Ziwa Kanas katika Eneo la Altay, Mkoa wa Xinjiang, China wakati wa majira ya mpukutiko
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma