Lugha Nyingine
Taasisi za fedha za kimataifa zaongeza makadirio ya ukuaji wa uchumi wa China kwa mwaka 2023
Taasisi za fedha za kimataifa zimeongeza makadirio yao ya ukuaji wa uchumi wa China kwa Mwaka 2023 baada ya uchumi wa nchi hiyo kukua kwa kasi kuliko ilivyotarajiwa katika robo ya tatu ya mwaka huu.
Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa, Kundi la Benki za Citigroup linakadiria pato la ndani la China kukua kwa asilimia 5.3 kutoka asilimia 5 ya awali.
Kampuni ya JP Morgan imekadiria uchumi wa China utakua kwa asilimia 5.2 mwaka huu, ikiwa ni makadirio ya zaidi ya asilimia 5, huku kampuni ya Morgan Stanley ikiongeza makadirio ya ukuaji wa uchumi wa China kwa asilimia 5.1 kutoka asilimia 4.8 mpaka 4.9 ya awali.
Benki ya UBS ya nchini Uswisi imeongeza makadirio ya ukuaji wa uchumi wa China mpaka asilimia 5.2, ikiwa ni alama 0.4 zaidi ya makadirio ya awali.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma