Lugha Nyingine
Teknolojia za kidijitali zahimiza?ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja
Wageni wakionekana kwenye eneo la maonyesho ya uchumi wa dijitali la Maonesho ya Sita ya China na Nchi za Kiarabu huko Yinchuan, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wahui wa Ningxia, Kaskazini-Magharibi mwa China, Septemba 22, 2023. Yakiwa yalifanyika kwa mara ya kwanza Mwaka 2013, Maonesho ya China na Nchi za Kiarabu yamekuwa jukwaa muhimu kwa China na Nchi za Kiarabu kuhimiza ushirikiano wa kivitendo na kuendeleza ushirikiano wa kiwango cha juu kujenga pamoja Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja. (Xinhua/Feng Kaihua) |
SHIJIAZHUANG – Katika karakana ya kampuni ya samani ya Mji wa Handan, Mkoa wa Hebei, Kaskazini mwa China, safu za vyuma tambarare vilivyoviringishwa vyenye unene wa milimita 0.6 tu vilikuwa vikichakatwa na kuwa bidhaa kama vile kabati za vitabu zenye kutumia teknolojia za akili bandia baada ya michakato mingi kama vile kukata, kugonga mihuri, kuchomelewa kwa umeme na kupuliziwa rangi.
"Michakato hii changamano hukamilishwa chini ya udhibiti wa vifaa vya kidijitali, kama vile mashine za kupinda kiotomatiki, ambazo huinua ufanisi wa uzalishaji na ubora wa samani kwa kiasi kikubwa, na huongeza nguvu za ushindani wa sokoni za bidhaa zetu," Zhang Baixiang, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Samani ya Steelite amesema.
Amesema kampuni yake kila mwaka inazalisha zaidi ya seti milioni 1 za aina mbalimbali za samani za chuma, ambazo huuzwa kwa nchi na maeneo zaidi ya 50 yanayoshiriki ujenzi wa pamoja wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI).
Teknolojia za kidijitali pia zimeleta mapinduzi makubwa katika uzalishaji na uuzaji wa bidhaa zinazozalishwa za Kampuni ya Dawa na Vifaa Tiba ya Chenguang huko Handan. Data za muda halisi kwenye skrini ya kompyuta hurekodi taarifa za uzalishaji na uuzaji bidhaa za kampuni hiyo. Sasa kwa usaidizi wa teknolojia ya data kubwa, kampuni hiyo inaweza kufikia data yoyote ya kampuni tanzu hata za mbali kama vile India, zinazohusiana na mambo kama vile kiasi cha malighafi, au kiasi cha pigmenti ya bidhaa zake.
"Teknolojia za kidijitali zimehimiza mageuzi na uboreshaji wa viwanda vya jadi, kusababisha kutokea kwa biashara ya mtandaoni ya kuvuka mipaka, mambo ya kifedha ya kimataifa, masoko ya kidijitali na aina nyingine za biashara, na kuhimiza maeneo mapya ya ukuaji wa uchumi," amesema Zhong Zeyu, Makamu wa Rais na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Biashara za Huduma la China.
Ikiwa na makao yake katika Mji wa Langfang, Hebei, kampuni ya usimamizi wa mnyororo wa ugavi ya Jiajia imetengeneza kwa kujitegemea jukwaa la huduma ya biashara ya nje.
"Kuanzia Januari hadi Agosti, kiasi cha thamani ya mauzo ya nje ya kampuni yetu ilifikia dola za Kimarekani milioni 180. Mauzo ya nje kwa nchi na maeneo ya BRI yalichukua zaidi ya asilimia 20 ya kiasi hiki," amesema Zhang Wen, meneja mkuu wa kampuni hiyo.
Zhang ameongeza kuwa kampuni hiyo imeanzisha maghala ya ng'ambo katika nchi na maeneo kadhaa ya BRI, yenye eneo lenye ukubwa wa jumla wa mita za mraba 90,000.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma