Lugha Nyingine
Matumizi thabiti katika?manununuzi wakati wa likizo yaonyesha uhai wa uchumi wa China unaoleta matumaini
Watu wakitembelea duka la bidhaa zisizotozwa ushuru huko Haikou, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Septemba 29, 2023. Mji wa Haikou umerekodi mauzo ya bidhaa zisizotozwa ushuru yenye thamani ya yuan bilioni 1.33 (kama dola milioni 182.2 za Kimarekani) wakati wa siku nane za likizo ya Sikukuu ya jadi ya Mbalamwezi na Sikukuu ya Taifa la China. (Xinhua/Pu Xiaoxu)
BEIJING - Chini ya jua lenye joto vuguvugu la majira ya mpukutiko, milima mirefu hutanda na misafara ya ngamia na watalii hutapakaa kwa urefu wa maili kwenye eneo la mandhari nzuri la Chemchemi ya Yueya katika Mji wa Dunhuang, Mkoa wa Gansu, Kaskazini-Magharibi mwa China.
Kwa mujibu wa takwimu kutoka idara ya utamaduni na utalii ya mji huo, katika likizo ya siku nane ya Sikukuu ya jadi ya Mbalamwezi na Sikukuu ya Taifa la China iliyomalizika Ijumaa, Dunhuang ilikaribisha watalii 667,700, sawa na ongezeko la zaidi ya mara kumi ikilinganishwa na mwaka uliopita.
"Takriban watalii 200,000 wamejionea uzuri wa mandhari ya kaskazini-magharibi katika Mlima Mingsha na Chemchemi ya Yueya, ziwa lenye umbo la mwezi mpevu lililozungukwa na matuta makubwa ya mchanga," amesema Wang Youxia, Naibu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Maendeleo ya Utalii ya Mlima Mingsha na Chemchemi ya Yueya ya Dunhuang.
Kufurika kwa watalii
Safari za abiria za wastani wa milioni 57.28 kila siku zilifanywa wakati wa likizo hiyo, ikiwa ni ongezeko la asilimia 57.1 kutoka likizo ya Sikukuku ya Taifa la China ya mwaka jana. Kuanzia Septemba 29 hadi Oktoba 6, idadi ya safari za abiria ilifikia milioni 458, Wizara ya Uchukuzi ya China imesema Jumamosi.
Wakati wa likizo hiyo, Mji wa Beijing ulikaribisha wageni milioni 11.88, ikiwa ni ongezeko la asilimia 12.9 ikilinganishwa na Mwaka 2019, kwa mujibu wa ofisi ya utamaduni na utalii ya mji huo. Mapato yatokanayo na shughuli za utalii za mji huo katika kipindi hicho yalifikia jumla ya yuan bilioni 15.57 (dola za kimarekani bilioni 2.16), ikiwa ni ongezeko la mara mbili ya kiasi kilichopatikana mwaka jana na ongezeko la asilimia 21.9 ikilinganishwa na takwimu za Mwaka 2019.
Matumizi mengi katika manunuzi wakati wa likizo
Sehemu zenye Vivutio maarufu vya utalii zilianzisha shughuli nyingi, ambazo maeneo ya biashara ya katikati ya miji yalishuhudia mauzo yakiongezeka, na filamu mpya zimetolewa wakati wa likizo. Mapato ya shughuli za utalii wa ndani yalipanda hadi yuan bilioni 753.43, na mapato ya kuangalia filamu kwenye majumba ya sinema ya China wakati wa likizo yalizidi yuan bilioni 2.7.
Mbali na maeneo makubwa yenye mandhari nzuri, maduka ya bidhaa zisizotozwa ushuru katika mkoa wa Hainan, Kusini mwa China pia yalinufaika kutokana na shughuli za utalii. Mji Mkuu wa mkoa huo Haikou, umerekodi mauzo ya bidhaa zisizotozwa ushuru yenye thamani ya yuan bilioni 1.33, ikiwa ni ongezeko la hadi asilimia 117 kuliko mwaka jana, imesema Idara ya Forodha ya Haikou. Idadi ya wateja wa bidhaa zisizotozwa ushuru ilifikia 170,000, sawa na ongezeko la asilimia 143 ikilinganishwa na kipindi kama hicho Mwaka 2022.
"Matumizi katika manunuzi wakati wa safari za likizo yameongezeka kwa kiasi kikubwa, ikionyesha uimara wa ukuaji wa uchumi wa China na matumaini yake ya maendeleo," amesema Zhao Xijun, profesa wa fedha katika Chuo Kikuu cha Umma cha China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma