Lugha Nyingine
Wamiliki wa meli Zanzibar waingiwa wasiwasi wakati Mwekezaji AGL akichukua mamlaka ya usimamizi wa shughuli za bandari ya Malindi
Wamiliki wa meli visiwani Zanzibar, Tanzania wamelalamikia mabadiliko ya taratibu na gharama baada ya serikali kukabidhi mamlaka ya usimamizi wa shughuli za Bandari ya Malindi kwa kampuni ya uwekezaji kutoka Ufaransa.
Jumatatu, Shirika la Bandari Zanzibar lilikabidhi mamlaka ya usimamizi wa bandari hiyo kwa Kampuni ya Africa Global Logistics (AGL), huku ikitarajia kuongezeka kwa ufanisi na mapato ya bandari hiyo.
Siku chache baada ya kuchukua mamlaka, wamiliki wa meli wamelalamikia kubadilishiwa taratibu za kutia nanga na malipo, hatua ambayo wanasema itaongeza gharama za uagizaji bidhaa.
Waendeshaji wa Majahazi wamelalamika kuwa ada zimeongezeka karibu maradufu tangu mwendeshaji mpya huyo wa bandari kuanza kufanya kazi.
Hata hivyo maafisa wa serikali wametetea ada hizo mpya wakisema ziliwekwa tangu mwaka 2018 lakini zilikuwa bado hazijatekelezwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma