Lugha Nyingine
Ushirikiano wa BRI waifanya Dunia kuwa ya kijani zaidi
Picha hii iliyopigwa Septemba 22, 2023 ikionyesha Baraza la Uchumi la Ulaya na Asia la 2023 huko Xi'an, Mji Mkuu wa Mkoa wa Shaanxi, Kaskazini-Magharibi mwa China. Kongamano la Kiuchumi la Ulaya na Asia la mwaka 2023 (EAEF) lenye mada ya kutafuta fursa za ushirikiano na maendeleo ya siku za baadaye, limefunguliwa Ijumaa huko Xi'an, Mji Mkuu wa Mkoa wa Shaanxi, Kaskazini-Magharibi mwa China. (Xinhua/Shao Rui)
XI'AN – Ikikabiliana na upepo mkali na jua, misafara ya ngamia ilitembea kwenye Njia ya kale ya Hariri, ikichukua hariri na chai kutoka China hadi Asia ya Kati na Ulaya zaidi ya miaka 1,000 iliyopita. Sasa, bidhaa za nishati safi huwasilishwa kwa nchi zinazojenga pamoja Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) kupitia treni na ndege za mizigo, na kugeuza upepo na jua kuwa hazina.
Wakati maendeleo ya kijani yanakuwa sasa makubaliano ya kimataifa, kampuni zaidi za China zimekuwa nguvu kubwa katika kujenga ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja usiotoa uchafuzi kwa mazingira.
Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 10 tangu kutolewa kwa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI).
Kwenye Baraza la Uchumi la Ulaya na Asia la 2023, Nikolay Pomoshchnikov, mkuu wa ofisi ya kanda ndogo kwa ajili ya Asia ya Kaskazini na Kati ya Kamati ya Uchumi na Jamii ya Asia Pasifiki ya Umoja wa Mataifa, amesema kuwa Asia ya Kati ina uwezo mkubwa wa nishati mbadala ikiwa ni pamoja na nishati ya jua, nishati ya upepo na umeme unaotokana na maji na kongamano hilo linatoa fursa nzuri sana kwa ushirikiano na China na nchi hizi.
Baraza hilo lililofanyika kwa siku tatu limehitimishwa Jumapili huko Xi'an, Mji Mkuu wa Mkoa wa Shaanxi Kaskazini Magharibi mwa China.
Xi'an, pia ni mahali pa kuanzia Njia ya Hariri ya kale, imeshuhudia maendeleo ya kijani kupitia mawasiliano ya kibiashara kati ya China na pande washirika wa BRI.
Mwishoni mwa Mwezi Aprili mwaka huu, mji huo ulizindua treni ya kwanza ya mizigo kutoka China na Ulaya kwa ajili ya usafirishaji wa magari yanayotumia nishati mpya (NEVs). Takwimu zilitolewa na Shirikisho la Viwanda la China zinaonyesha kuwa kuanzia Januari hadi Agosti 2023, China imeuza nje magari yanayotumia nishati mpya zaidi ya 727,000, ikiwa ni ongezeko la mara 1.1 kuliko wakati kama huo wa mwaka uliopita.
Mwezi uliopita, treni iliyopakia moduli za vifaa vya nishati ya jua (PV) iliondoka Xi'an kuelekea Tashkent, Uzbekistan. Moduli hizi zitatumika kwenye mradi wa nishati ya jua (PV) wa gigawati 1 nchini Uzbekistan, ambao utazalisha nishati safi yenye uwezo wa kWh bilioni 2.4 kila mwaka, na kusaidia kupunguza utoaji wa kaboni kwa tani hadi milioni 2.4.
Adil Ahmed, kutoka Pakistan, amehisi maendeleo ya nishati safi katika mji wa asili yake. Ahmed, mwonyeshaji bidhaa aliyeshiriki kwenye maonyesho ya uchumi na biashara yaliyofanyika pembezoni mwa baraza hilo la Xi'an, amesema Pakistan ina rasilimali nyingi za nishati ya jua, ambazo zinafaa kwa kuendeleza umeme wa jua.
"Nimeweka paneli za PV kwenye paa la nyumba yangu ," amesema mzee huyo wa miaka 65, huku akiongeza kuwa paneli nyingi zimetengenezwa nchini China.
Watu wakitazama magari yanayotumia nishati mpya kwenye Maonyesho ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Kibiashara ya EAEF & Maonyesho ya Bidhaa za Uuzaji na Uingizaji ya China (Shaanxi) mjini Xi'an, Mji Mkuu wa Mkoa wa Shaanxi, Kaskazini-Magharibi mwa China, Septemba 22, 2023. (Xinhua/Shao Rui)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma