久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

China yaongoza msukumo wa kimataifa kwa ajili ya ukuaji endelevu na jumuishi wa uchumi katika UNGA

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 22, 2023

UMOJA WA MATAIFA - China imeahidi kuhimiza zaidi Pendekezo la Maendeleo ya Dunia (GDI) na utekelezaji wa Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ya Mwaka 2030 katika Mkutano wa Baraza Kuu la 78 la Umoja wa Mataifa (UNGA) uliofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani wiki hii.

Makamu wa Rais wa China Han Zheng amesisitiza Ahadi ya China ya kusukuma maendeleo endelevu na jumuishi kupitia ushirikiano wa pande zote wa kimataifa wakati aliposhiriki katika Mjadala Mkuu wa UNGA na shughuli muhimu, ikiwa ni pamoja na Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa SDG na mkutano wa ngazi ya juu wa Matokeo ya Ushirikiano wa Pendekezo la Maendeleo ya Dunia ulioandaliwa na China, pamoja na mazungumzo ya pande mbili.

Shughuli hizo zimejiri katika wakati muhimu ambapo maendeleo endelevu yako hatarini, na maendeleo kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu yamekwama huku kukiwa na kudorora kwa uchumi na kuongezeka kwa mashindano ya siasa za kijiografia.

Akihutubia Mkutano wa SDG, Han amesema China inataka kuunganisha utekelezaji wa Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu na mikakati ya kitaifa ya maendeleo ya muda wa kati na mrefu, na daima inaunganisha maendeleo yake na ustawi na utulivu wa kimataifa.

Kwa ajili hiyo, Han ametoa mapendekezo manne ya China: kuweka kithabiti maendeleo katikati ya ajenda ya Dunia , kujenga uchumi wa dunia ulio wazi, kuchukua fursa ya kihistoria ya duru mpya ya mapinduzi ya sayansi na teknolojia, na kuendeleza uhusiano wa wenzi wa maendeleo ya Dunia,

“China itajitolea bila kuyumbayumba kufanyia kazi malengo mawili ya kufikia kilele cha utoaji wa hewa ya kaboni na usawazishaji wa hewa ya kaboni,” Han amesema alipokutana na John Kerry, Mjumbe Maalumu wa Rais wa Marekani kuhusu Tabianchi pembezoni mwa UNGA.

Amesema, licha ya kuchangia ukuaji wa uchumi wa Dunia kwa kasi na hekima yake ya maendeleo, China, kama ilivyofanya siku zote , inachanganua kikamilifu maono na mapendekezo mapya pamoja na nchi nyingine kwa ajili ya mustakabali bora na endelevu kwa pamoja.

Kama sehemu nyingine ya shughuli za Umoja wa Mataifa wiki hii, mkutano wa ngazi ya juu kuhusu Matokeo ya Ushirikiano wa GDI uliandaliwa na China siku ya Jumanne ili kuhakiki manufaa ya awali ya ushirikiano na maelewano ya pamoja kwa ajili ya kujitolea zaidi kwa GDI.

“China iko tayari kushirikiana na pande zote kusukuma mbele maendeleo thabiti ya GDI,” Han amesema.

Hasa miaka miwili iliyopita, Septemba 21, 2021, Rais Xi Jinping wa China alileta dhana hiyo ya maendeleo kwenye mjadala mkuu wa Mkutano wa Baraza Kuu la 76 la Umoja wa Mataifa, na baadaye dhana hiyo ilibadilika kuwa dhana ya kiumma duniani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>