久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

Benki ya China (BOC) yafungua tawi lake katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 07, 2023

Liu Jin, Mkuu wa Benki ya China (BOC), akihutubia hafla ya ufunguzi wa tawi la benki hiyo mjini Riyadh, Saudi Arabia, Septemba 5, 2023. (Xinhua/Wang Haizhou)

Liu Jin, Mkuu wa Benki ya China (BOC), akihutubia hafla ya ufunguzi wa tawi la benki hiyo mjini Riyadh, Saudi Arabia, Septemba 5, 2023. (Xinhua/Wang Haizhou)

RIYADH - Benki ya China (BOC) imefungua tawi lake katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh siku ya Jumanne ili kupanua mtandao wake wa huduma za kifedha katika nchi hiyo ya Kiarabu.

Akihutubia hafla ya ufunguzi wa tawi hilo, Mkuu wa BOC Liu Jin amesema kuanzishwa kwa tawi hilo, ambalo ni njia ya biashara na uwekezaji kati ya China na Saudi Arabia, kunaonyesha dhamira ya dhati ya kuendeleza ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo mbili.

Liu ameongeza kuwa BOC iko imara katika kutumia huduma zake za kimataifa ili kuendelea kuimarisha mtandao wake wa huduma duniani kote, ikiwa ni pamoja na nchi za Kiarabu, na kuchangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu.

Gavana wa Benki Kuu ya Saudi Arabia Ayman Al-Sayari, kwa upande wake, amesema ufunguzi wa tawi la BOC mjini Riyadh ni wakati muhimu sana katika kuimarisha ushirikiano wa kivitendo kati ya China na Saudi Arabia, akieleza uungaji mkono usioyumba wa nchi yake kwa ajili ya ukuaji endelevu na maendeleo endelevu ya BOC katika nchi hiyo

Kwenye hafla hiyo, Balozi wa China nchini Saudi Arabia Chen Weiqing ametoa pongezi kwa uzinduzi wa tawi hilo akisema unawakilisha hatua mpya ya ushirikiano wa kifedha kati ya China na Saudi Arabia.

Naibu Waziri wa Uwekezaji wa Saudi Arabia, Saleh Ali Khabti amesema kuanzishwa kwa tawi hilo ni hatua muhimu katika kukidhi mahitaji ya huduma za kifedha kwa wateja wa hali ya juu kutoka nchi zote mbili, ambao wanatafuta huduma kutoka kwa taasisi za benki za China.

Naibu waziri huyo ameeleza matumaini katika uwezo wa tawi hilo kupata ustawi thabiti katika soko la Saudi Arabia, kuhakikisha ufanisi thabiti, na kuwezesha ushirikiano wa uwekezaji baina ya nchi hizo.

Kwa kufunguliwa tawi hilo la Riyadh, BOC sasa inafanya kazi na kutoa huduma za kifedha katika nchi na maeneo 64 duniani kote.?

Balozi wa China nchini Saudi Arabia Chen Weiqing, akihutubia hafla ya ufunguzi wa tawi la Benki ya China (BOC) mjini Riyadh, Saudi Arabia, Septemba 5, 2023. (Xinhua/Wang Haizhou)

Balozi wa China nchini Saudi Arabia Chen Weiqing, akihutubia hafla ya ufunguzi wa tawi la Benki ya China (BOC) mjini Riyadh, Saudi Arabia, Septemba 5, 2023. (Xinhua/Wang Haizhou)

Wageni waalikwa wakihudhuria hafla ya ufunguzi wa tawi la Benki ya China (BOC) mjini Riyadh, Saudi Arabia, Septemba 5, 2023. (Xinhua/Wang Haizhou)

Wageni waalikwa wakihudhuria hafla ya ufunguzi wa tawi la Benki ya China (BOC) mjini Riyadh, Saudi Arabia, Septemba 5, 2023. (Xinhua/Wang Haizhou)

Gavana wa Benki Kuu ya Saudi Arabia, Ayman Al-Sayari, akihutubia hafla ya ufunguzi wa tawi la Benki ya China (BOC) mjini Riyadh, Saudi Arabia, Septemba 5, 2023. (Xinhua/Wang Haizhou)

Gavana wa Benki Kuu ya Saudi Arabia, Ayman Al-Sayari, akihutubia hafla ya ufunguzi wa tawi la Benki ya China (BOC) mjini Riyadh, Saudi Arabia, Septemba 5, 2023. (Xinhua/Wang Haizhou)

Naibu Waziri wa Uwekezaji wa Saudi Arabia, Saleh Ali Khabti, akihutubia hafla ya ufunguzi wa tawi la Benki ya China (BOC) mjini Riyadh, Saudi Arabia, Septemba 5, 2023. (Xinhua/Wang Haizhou)

Naibu Waziri wa Uwekezaji wa Saudi Arabia, Saleh Ali Khabti, akihutubia hafla ya ufunguzi wa tawi la Benki ya China (BOC) mjini Riyadh, Saudi Arabia, Septemba 5, 2023. (Xinhua/Wang Haizhou)

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>