Lugha Nyingine
Viashiria mbalimbali vyaonyesha uthabiti na nguvu ya uchumi wa China
Picha hii iliyopigwa Julai 3, 2023 ikionyesha mikono ya roboti ikifanya kazi kwenye karakana ya uchomeleaji ya Kampuni ya Magari yanayotumia nishati mpya ya GAC Aion huko Guangzhou, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China. (Xinhua/Deng Hua)
BEIJING - Wakati changamoto kali zikiendelea kuchochea wasiwasi juu ya matarajio ya ukuaji wa uchumi duniani, viashiria mbalimbali vimeonyesha uthabiti na nguvu ya uchumi wa China.
Katika nusu ya kwanza ya mwaka (H1), China ilirekodi upanuzi wa Pato la Taifa (GDP) wa asilimia 5.5, ikiwa ni wa kasi zaidi miongoni mwa nchi zenye uchumi mkubwa duniani. Ufanisi huu mkubwa umetokana na ukuaji thabiti wa viashirio vikuu vya uchumi katika miezi saba ya kwanza ya Mwaka 2023, huku uzalishaji wa bidhaa zenye thamani ya nyongeza za viwanda na mauzo ya rejareja ya bidhaa za matumizi vikiendelea kuongezeka kwa hatua madhubuti .
Tangu robo ya pili ya mwaka, mashirika na taasisi kadhaa za kimataifa zimerekebisha makadirio yao ya ukuaji wa uchumi wa China mwaka huu kwenda juu. Benki ya Dunia, kwa mfano, imepandisha makadirio ya ukuaji wa uchumi wa China hadi asilimia 5.6 mwezi Juni kutoka makadirio ya Januari ya asilimia 4.3.
Mbali na msingi imara wa kiuchumi, China pia imepata ukuaji katika maeneo muhimu kama vile usambazaji wa nafaka na nishati.
Uzalishaji wa nafaka nchini China kwa mwaka umeongezeka kwa zaidi ya kilo bilioni 650 katika miaka ya hivi karibuni, wakati uzalishaji wake wa nishati ulipanda kwa asilimia 3.8 kutoka kiwango cha mwaka jana katika kipindi cha Januari-Julai.
Maendeleo ya sekta zinazoibukia zenye umuhimu wa kimkakati, ambayo yanaonekana kama vichocheo vipya vya ukuaji uchumi na wachambuzi, pia yameshika kasi katika miezi saba ya kwanza ya mwaka huu, kama inavyoshuhudiwa kwenye ukuaji wa kasi katika sekta ya teknolojia ya hali ya juu na viwanda vya utengenezaji wa vifaa.
Hasa, mauzo ya magari yanayotumia nishati mpya yaliongezeka zaidi ya mara mbili katika miezi saba ya kwanza hadi kufikia bidhaa 636,000, ikiwa ni ufanisi wa kutia moyo dhidi ya hali mbaya ya biashara ya kimataifa.
Gu Yan, mtafiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maendeleo na Mageuzi ya Kina ya China (NDRC), ameeleza kuwa uvumbuzi kama msukumo wa msingi wa maendeleo umeimarika zaidi nchini China, akisema kuwa utarahisisha uboreshaji wa viwanda na kuhimiza kuibuka kwa mifumo mipya ya biashara.
Ili kuimarisha uhai wa biashara zaidi, Serikali ya China imesukuma mbele mageuzi, na kutangaza mwongozo wenye hatua 31 ili kuimarisha uchumi wa kibinafsi na nyaraka inayolenga kufungua mlango zaidi .
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma