Lugha Nyingine
Makubaliano ya uwekezaji na biashara yenye thamani ya dola bilioni 72 yasainiwa kwenye maonyesho ya biashara ya Xinjiang, China
Washiriki wakitembelea eneo la maonyesho kwenye Maonyesho ya Bidhaa na Biashara ya Eurasia (nchini China) (EACT Expo) 2023 huko Urumqi, Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang, Kaskazini-Magharibi mwa China, Agosti 17, 2023. (Xinhua/Wang Fei)
URUMQI - Makubaliano 360 ya uwekezaji na biashara yametiwa saini kwenye Maonyesho ya Bidhaa na Biashara Eurasia (nchini China) Mwaka 2023 katika Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur, Kaskazini Magharibi mwa China, waandaaji wamesema Jumatano.
Mikataba hiyo ni yenye thamani ya jumla ya yuan bilioni 521 (kama dola za kimarekani bilioni 72.4), huku maonyesho hayo yakishuhudia uwepo wa eneo kubwa zaidi la maonyesho na idadi ya waonyeshaji wa kimataifa, Xing Tao, mkuu wa idara ya biashara ya mkoa huo, ameuambia mkutano na waandishi wa habari.
Kampuni zaidi ya 1,300 zimeshiriki maonyesho ana kwa ana, na 4,600 zaidi zimeshiriki katika maonyesho ya mtandaoni. Waandaaji wameandaa shughuli 64 za kutangaza biashara za viwanda vikubwa vya China, kama vile uchimbaji madini bila kuchafua mazingira, nafaka na mafuta, pamba, mavazi na nguo.
Jumla ya wafanyabiashara 18,700, wakiwemo zaidi ya 1,000 wa kimataifa, wameshiriki katika maonyesho hayo. Wageni, wafanyabiashara na wasomi mashuhuri zaidi ya 800 kutoka nchi na maeneo 40, pamoja na mashirika saba ya kimataifa, wamehudhuria maonyesho hayo.
Maonyesho hayo yamefanyika Urumqi, mji mkuu wa Xinjiang, kuanzia Agosti 17 hadi 21, na kuvutia watembeleaji zaidi ya 100,000, huku mauzo ya bidhaa zilizoonyeshwa kwenye eneo husika yakizidi Yuan milioni 100.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma