Lugha Nyingine
China yasisitiza uungaji mkono zaidi wa kifedha kwa uchumi halisi, na kupunguza hatari za deni
Picha iliyopigwa Oktoba 19, 2020 ikionyesha mandhari ya nje ya Benki kuu ya China hapa Beijing, China. (Xinhua/Peng Ziyang)
BEIJING - Mamlaka za kifedha za China zimesisitiza juhudi za kuimarisha uungaji mkono wa kifedha kwa uchumi halisi, na pia kuzuia na kupunguza hatari za deni la serikali za mitaa nchini China.
“Uungaji mkono wa kifedha kwa uchumi halisi unapaswa kuwa na nguvu, madhubuti, wenye muundo bora na bei endelevu,” imesema Benki kuu ya China katika taarifa iliyotolewa Jumapili baada ya mkutano wa pamoja na Idara ya Kitaifa ya Udhibiti wa Fedha ya China na Kamati ya Udhibiti wa Dhamana ya China.
Kuimarika kwa uchumi wa China kumekuwa na maendeleo kama wimbi na mchakato wenye changamoto, kwa mujibu wa taarifa hiyo, ambayo imehimiza juhudi za kusukuma mbele kuboresha uchumi wenye ufanisi, nguvu ya kiasili ya kuendesha uchumi na matarajio ya kijamii, na kupunguza hatari na hatari zilizojificha.
Katika mkutano huo, China imeapa kuimarisha uungaji mkono wa mikopo kwa biashara ndogo na za kati pamoja na sekta kama vile maendeleo ya kijani, uvumbuzi wa teknolojia na viwanda, ukarabati na ujenzi upya wa vijiji vilivyoko mijini na ujenzi wa miundombinu ya umma ambayo inaweza kutumika katika maisha ya kila siku na kwa dharura.
Pia imeahidi kufanya uungaji mkono wa kifedha kwa uchumi halisi kuwa endelevu zaidi, na kuhakikisha kuwa sekta ya fedha inakuwa na jukumu chanya katika kuongeza matumizi kwenye manunuzi, kuleta utulivu wa uwekezaji na kupanua mahitaji ya ndani.
Kwenye mkutano huo, mamlaka hizo za kifedha zimeahidi kufanya jitihada za kuimarisha zana za sera na hatua za kuzuia na kupunguza hatari za madeni, huku zikiimarisha taratibu za kufuatilia, kutathmini, kuzuia na kudhibiti hatari, na kusukuma mbele kazi ya udhibiti wa hatari katika mikoa muhimu ili kulinda kikamilifu msingi wa kutokuwa na hatari za kimfumo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma