Lugha Nyingine
Mauzo ya nje ya nchi ya chai ya Kenya yapungua
(CRI Online) Agosti 15, 2023
Bodi ya Chai Kenya (TBK) imesema mauzo ya chai ya Kenya nje ya nchi yameathiriwa na migogoro inayoendelea nchini Sudan na kati ya Russia na Ukraine, ambapo thamani ya mauzo yake ya nje ya nusu mwaka ilipungua wakati bei yake duniani ikiendelea kuwa chini.
Bodi hiyo imesema kipindi kinachoishia Juni ya mwaka huu, Kenya imeuza nje chai yenye uzito wa tani laki 1.91 ikiwa na thamani ya takriban dola za kimarekani milioni 432, ikilinganishwa na chai yenye uzito wa tani laki 2.43 yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 614 mwaka jana kipindi kama hicho. Imeongeza kuwa pungufu ya asilimia 29 ya thamani ya chai inatokana na mahitaji ya chai ya Kenya kupungua duniani yakiathiriwa na migogoro.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma