Lugha Nyingine
Baraza la serikali la China lasisitiza kuboresha mazingira ya uwekezaji kutoka nje
Watu wakiwa kwenye maonyesho ya kukutanisha wafanyabiashara kwenye Maonyesho ya 6 ya Kimataifa ya Uagizaji bidhaa ya China (CIIE) katika Kituo cha taifa cha Maonyesho na Mikutano mjini Shanghai China, Julai 26, 2023. Maonesho ya 6 ya CIIE yamepangwa kufanyika mjini Shanghai kuanzia Nov. 5 hadi 10. (Xinhua/Xin Mengchen)
Baraza la serikali la China limetoa taarifa ikiwa na miongozo kuhusu kuboresha mazingira ya uwekezaji wa kigeni na kuimarisha juhudi za kuvutia wawekezaji kutoka nje.
Katika taarifa yake yenye miongozo hiyo, hatua 24 mahsusi zimetajwa katika vipengele sita zikiwa ni vipaumbele.
Vipaumbele hivyo ni pamoja na kuboresha matumizi ya fedha za kigeni, kudhamini ushughulikiaji wa kitaifa kwa makampuni ya biashara ya kigeni, kuimarisha ulinzi wa uwekezaji kutoka nje, kuboresha uwezekano wa uwekezaji na utendaji, kuongeza msaada wa kifedha na kodi, na kuboresha njia za kuvutia uwekezaji wa kigeni.
Taarifa hiyo pia imesema mikoa yote inahimizwa kuchukua hatua zinazoendana kwa kuzingatia hali ya ndani ili kuimarisha usawa wa sera.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma