Lugha Nyingine
Thamani ya mauzo ya bidhaa zisizotozwa kodi Hainan kati ya Januari na Julai mwaka huu yafikia Yuan bilioni?28.93
Watalii wakinunua bidhaa kwenye eneo linalouza bidhaa zisizo na kodi mjini Haikou, Mkoani Hainan kusini mwa China, Julai 12, 2023. (Xinhua/Yang Guanyu)
HAIKOU, Agosti 8 (Xinhua)
Mkoa wa Hainan ulioko Kusini mwa China umeweka rekodi ya jumla ya mauzo ya bidhaa zisizotozwa kodi ya yuan bilioni 28.93 (sawa na dola bilioni 4 za Kimarekani) katika miezi saba ya kwanza ya mwaka huu.
Idara ya forodha ya mji wa Haikou imesema kuanzia mwezi Januari hadi Julai, karibu wateja milioni 4.2 walinunua zaidi ya bidhaa milioni 34 zisizotozwa kodi katika mkoa huo.
Kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu, mkoa wa Hainan ulitangaza hatua mbalimbali za kuongeza kihimiza matumizi kwenye bidhaa zisizotozwa kodi. Hatua hizi ni pamoja na kutoa kuponi milioni 20 kwa ajili ya manunuzi ya bidhaa zisizotozwa kodi, kufanya tamasha la kimataifa la manunuzi ya bidhaa zisizotozwa kodi, na kuhimiza sera ya kuuza bidhaa zisizotozwa kodi nje ya mkoa. Maduka yasiyolipishwa kodi katika kisiwa hicho yamefanya matangazo zaidi ya 30 ya kununua bidhaa mtandaoni na nje ya mtandao.
Tangu Aprili 20 mwaka 2021 mkoa wa Hainan ulipotoa sera inayowaruhusu watalii wa ndani kununua bidhaa katika kisiwa hicho bila kutozwa kodi, marekebisho kadhaa ya sera yamefanyika.
Marekebisho ya kuanzia tarehe 1 Julai 2020, yaliongeza ukomo wa ununuzi wa bidhaa zisizotozwa kodi cha kila mwaka kutoka kwa yuan 30,000 hadi yuan 100,000 kwa kila mtu, na kupanua aina kuu za bidhaa zisizotozwa kodi kutoka 38 hadi 45.
Mwezi Juni mwaka 2020 China ilitangaza mpango kukifanya kisiwa cha Hainan kuwa eneo la biashara huria lenye ushawishi mkubwa duniani, na la kiwango cha juu kabla ya kufika katikati ya karne hii. Katika miaka ya hivi karibuni, mkoa wa Hainan umekuwa kivutio cha manunuzi kwa wateja mbalimbali wa China.
Kupitia miaka ya juhudi za kuimarisha utalii wa ndani na shughuli za manunuzi, kisiwa cha Hainan sasa kina jumla ya maduka 12 yanayouza bidhaa zisizotozwa kodi.
Habari ya Picha: Mandhari Nzuri ya Mbuga ya Milimani huko Yunnan, China
Wakulima washughulikia kuvuna mazao ya mbegu za mayungiyungi huko Wilaya ya Quannan, Mkoa wa Jiangxi
Panda "Ruyi" na "Dingding" washerehekea siku ya kuzaliwa huko Moscow
Safari isiyoweza kusahaulika ya mcheza dansi wa Russia katika Mkoa wa Xinjiang, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma