Lugha Nyingine
Akiba ya fedha za kigeni ya China kwa mwezi Julai yaongezeka
Picha inaonyesha karani akichagua noti ya dola kati ya noti za dola ya Marekani na Renminbi (RMB) kwenye benki moja huko Linyi, Shandong Mashariki mwa China. (Xinhua/Zhang Chunlei)
BEIJING, Agosti 7 (Xinhua)
Idara ya usimamizi wa fedha za kigeni ya China imetoa taarifa ikisema hadi kufikia mwezi Julai mwaka huu, akiba ya fedha za kigeni ya China iliongezeka na kufikia dola za Kimarekani trilioni 3.204 kutoka dola trilioni 3.193 za mwishoni mwa mwezi Juni.
Kutokana na athari ya sera za fedha na matarajio ya uchumi mkuu, data ya uchumi mkuu wa dunia na mambo mengine, katika mwezi wa Julai faharisi ya dola ya Marekani ilipungua na thamani ya mali ya kifedha duniani ilipanda kwa ujumla. Idara hiyo imesema kutokana na tafsiri ya kiwango cha ubadilishaji wa fedha na mabadiliko ya bei ya mali, akiba ya fedha za kigeni ya China kwa mwezi Julai iliongezeka.
Taarifa ya idara hiyo pia imesema uchumi wa China umeonesha uthabiti mkubwa na uwezekano wa kuwa na maendeleo zaidi, na misingi yake mikuu haijabadilika, ambayo inafaa kudumisha utulivu wa kimsingi wa akiba ya fedha za kigeni.
Wakulima washughulikia kuvuna mazao ya mbegu za mayungiyungi huko Wilaya ya Quannan, Mkoa wa Jiangxi
Panda "Ruyi" na "Dingding" washerehekea siku ya kuzaliwa huko Moscow
Safari isiyoweza kusahaulika ya mcheza dansi wa Russia katika Mkoa wa Xinjiang, China
Mradi wa kuzalisha umeme kwa upepo wa De Aar nchini Afrika Kusini wapunguza utoaji wa hewa ya kaboni
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma