Lugha Nyingine
Biashara ya huduma nchini China imeongezeka kwa asilimia 8.5 katika miezi sita ya kwanza?ya mwaka huu
Abiria wanaingia kwenye eneo la wasafiri wa nje ya nchi kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sanya Phoenix huko Sanya, Mkoani Hainan kusini mwa China, Julai 26, 2023. (Xinhua/Yang Guanyu)
Takwimu kutoka wizara ya biashara ya China zilizotolewa hivi karibuni zinaonesha kuwa thamani ya biashara ya huduma nchini China imekuwa na ongezeko la asilimia 8.5 katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu.
Takwimu zinaonesha kuwa thamani ya biashara hiyo imefikia Yuan trilioni 3.14 (sawa na Dola za kimarekani bilioni 439.19).
Hata hivyo usafirishaji wa huduma nje ulipungua kwa asilimia 5.9 na thamani yake kufikia Yuan trilioni 1.32, na thamani ya uagizaji wa huduma ilikuwa Yuan trilioni 1.81, ikiwa ni ongezeko la asilimia 22.1 ikilinganishwa na mwaka mmoja uliopita.
Katika kipindi hicho, thamani ya biashara ya huduma ya China inayohitaji maarifa zaidi ilidumisha ukuaji wa kasi, na kuongezeka kwa asilimia 12.3 na thamani yake kufikia Yuan trilioni 1.36.
Katika kipindi hicho, huduma zinazohusiana na sekta ya usafiri zilionekana kurudi katika hali ya kawaida. Takwimu pia zinaonesha kuwa usafirishaji na uagizaji wa huduma za usafiri uliongezeka kwa asilimia 52.4 na asilimia 66.4 mtawalia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma