Lugha Nyingine
Biashara kati ya Kenya na nchi nyingine za Afrika yaongezeka huku wito ukitolewa wa muunganisho?wa kikanda
(CRI Online) Julai 18, 2023
Biashara kati ya Kenya na nchi nyingine za Afrika imefikia rekodi ya juu ya dola za kimarekani bilioni 1.18 katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka huu, ikilinganishwa na dola za kimarekani milioni 960 katika kipindi kama hicho Mwaka 2022.
Takwimu mpya zilizotolewa na Benki Kuu ya Kenya jana jumatatu zimeonyesha kuwa, ongezeko hilo limetokana na juhudi za serikali ya nchi hiyo katika kuboresha uhusiano wa pande nyingi na biashara kati ya nchi za Bara la Afrika.
Benki hiyo imesema, Mwaka 2022, mauzo ya bidhaa za Kenya kwa nchi nyingine za Afrika yalifikia dola za kimarekani bilioni 2.6, ikiwa imeongezeka kutoka dola bilioni 2.2 zilizopatikana Mwaka 2021.
(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma