Lugha Nyingine
Wauzaji magari nchini?Kenya wapinga ongezeko la asilimia 35?kwa magari yanayoagizwa kutoka nje ya nchi
Waagizaji wa magari nchini Kenya wamepinga uamuzi wa kuongeza ushuru hadi asilimia 35 kwa magari yanayotoka nje, wakisema viwango hivyo vipya vimetekelezwa bila kuwashirikisha kikamilifu.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Waagizaji Magari la Kenya, Peter Otieno amesema utekelezaji wa asilimia 35 ya ushuru wa forodha kwa wanunuzi wa magari nchini Kenya lazima usitishwe kwa sababu wahusika wa sekta hiyo hawakushauriwa na kushirikishwa kabla ya kutekelezwa, jambo ambalo ni kinyume na Katiba.
Ushuru huo mpya wa uagizaji magari hayo, una maana kwamba waagizaji wa magari wanapaswa kutathmini upya bei zao za mauzo ili kupanda kati ya Sh50,000 hadi Sh100,000 kwa aina ndogo za magari na zaidi ya Sh500,000 kwa magari makubwa na yanayotumia mafuta kwa wingi.
Wanunuzi wa magari nchini Kenya mapema mwezi huu waliongezewa asilimia 35 ya ushuru wa kuagiza magari kutoka nje ya nchi baada ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuidhinisha ombi la Kenya la kuongeza ushuru chini ya ushuru wa pamoja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma