Lugha Nyingine
Maonesho ya sabasaba yamalizika kwa mafanikio jijini Dar es Salaam
Rais wa Tanzania Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefunga rasmi Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu kama Sabasaba, ambayo yamefanyika kwa siku 16 na kuwataka wafanyabiashara wa ndani kuzalisha bidhaa zenye ubora wa juu kwa ajili ya masoko ya kikanda na kimataifa.
Amesema wafanyabiashara hao wanapaswa kujiandaa vyema kwa ajili ya soko jipya katika Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika (AfCFTA) na kuongeza kuwa amefurahishwa kuona bidhaa zilizoonyeshwa katika maonesho ya Sabasaba ya mwaka huu zina ubora wa juu.
Pia amewakumbusha wafanyabiashara wa ndani kuhusu changamoto za kutumia masoko ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).
Dkt. Mwinyi ambaye alikagua baadhi ya mabanda ameipongeza Taasisi ya Biashara na Usafirisaji Bidhaa ya Afrika Mashariki (EACLC), ambayo ni mdhamini mkuu wa maonesho ya Sabasaba kwa kufanikisha maonesho hayo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma