久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

Biashara ya nje ya China yaendeleza kuongezeka huku ikiwa na miundo bora zaidi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 14, 2023

Watu wakitembelea Maonyesho ya 133 ya Uagizaji na Uuzaji nje wa Bidhaa ya China, ambayo pia yanajulikana kama Maonyesho ya Canton, huko Guangzhou, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, Aprili 15, 2023. (Xinhua/Liu Dawei)

Watu wakitembelea Maonyesho ya 133 ya Uagizaji na Uuzaji nje wa Bidhaa ya China, ambayo pia yanajulikana kama Maonyesho ya Canton, huko Guangzhou, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, Aprili 15, 2023. (Xinhua/Liu Dawei)

BEIJING - Biashara ya nje ya China imedumisha ukuaji thabiti huku ikiwa na muundo bora zaidi na nguvu zaidi ya ushindani katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, ikihimili changamoto zilizoletwa na kudorora kwa kuimarika uchumi duniani, kuongezeka kwa hatari za siasa za kijiografia, na kudhoofika kwa mahitaji ya nje, takwimu rasmi za Idara Kuu ya Forodha ya China (GAC) zimeonyesha Alhamisi.

Idara hiyo imesema, thamani ya jumla ya bidhaa zinazoagizwa na kuuzwa nje ya China iliongezeka kwa asilimia 2.1 kuliko mwaka jana wakati kama huo na kufikia yuan trilioni 20.1 (sawa na dola trilioni 2.81 za Kimarekani).

“Ni mara ya kwanza kwa bidhaa za China zinazoagizwa na kuuzwa nje kuzidi thamani ya Yuan trilioni 20 katika kipindi cha mwezi Januari hadi Juni,” amesema msemaji wa GAC Lyu Daliang kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Takwimu zimeonyesha kuwa, mauzo ya bidhaa ya China kwa nchi za nje yalikua kwa asilimia 3.7 kuliko mwaka jana wakati kama huo na kufikia yuan trilioni 11.46 huku uagizaji wa bidhaa kutoka nje ukishuka kwa asilimia 0.1 kutoka mwaka uliotangulia hadi yuan trilioni 8.64.

Treni ya mizigo inayotoa huduma kati ya China na Ulaya iliyopakiwa magari ya chapa ya China ikingoja kuondoka kwenye kituo cha kimataifa cha kontena cha Harbin huko Harbin, Mji Mkuu wa Mkoa wa Heilongjiang Kaskazini-Mashariki mwa China, Aprili 16, 2023. (Xinhua/Zhang Tao)

Treni ya mizigo inayotoa huduma kati ya China na Ulaya iliyopakiwa magari ya chapa ya China ikingoja kuondoka kwenye kituo cha kimataifa cha kontena cha Harbin huko Harbin, Mji Mkuu wa Mkoa wa Heilongjiang Kaskazini-Mashariki mwa China, Aprili 16, 2023. (Xinhua/Zhang Tao)

Uagizaji na uuzaji nje wa bidhaa katika robo ya kwanza na ya pili ya mwaka huu ulifikia yuan trilioni 9.76 na yuan trilioni 10.34 mtawalia, huku zote ziliongezeka kuliko mwaka jana wakati kama huo, kwa mujibu wa takwimu hizo za GAC.

Katika kipindi hicho, muundo wa biashara ya nje wa China pia uliboreshwa katika aina za bidhaa na usambazaji wa kikanda.

Lyu amesema, biashara ya jumla, ambayo inahusisha minyororo mirefu zaidi ya viwanda na thamani ya juu zaidi, ilirekodi kiwango cha juu cha ukuaji kuliko biashara ya nje kwa jumla.

Thamani ya biashara ya jumla ilichukua asilimia 65.5 ya thamani yote ya biashara ya nchi nzima.

Mikoa ya kati na magharibi na mikoa ya kaskazini mashariki mwa China imeongeza kasi ya ufunguaji mlango, huku uagizaji na uuzaji wao bidhaa nje ya China ukiongezeka kwa asilimia 2.8 na asilimia 4.5, mtawalia. Thamani yao ya pamoja ilichangia asilimia 21 ya jumla ya nchi nzima.

Lyu amekiri bado kuna changamoto zinazoikabili China kwenye maendeleo ya biashara ya nje katika nusu ya pili ya mwaka, akibainisha kuwa mfumuko wa bei katika nchi zilizoendelea zenye uchumi mkubwa bado uko juu, migogoro ya siasa za kijiografia inaendelea, na mahitaji ya nje ya muda mfupi bado hakutoshi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>