Lugha Nyingine
Botswana yatumai kuuza nyama ya ng’ombe kwa China katika?muda mfupi ujao
(CRI Online) Julai 05, 2023
Waziri wa Kilimo wa Botswana Fidelis Molao, amesema Botswana inajipanga kuuza nyama bora ya ng’ombe kwa China katika kipindi cha muda mfupi ujao.
Akiongea nchini Botswana baada ya kurudi kutoka mjini Changsha katika Mkoa wa Hunan nchini China alikohudhuria Maonesho ya Tatu ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika, Bw. Molao amesema nchi hiyo inafanya juhudi na kutarajia kusaini makubaliano na China ili kuingia kwenye soko la nyama ya ng’ombe la China.
Ameongeza kuwa nchi hiyo pia inatarajia kuingia kwenye sekta ya mauzo ya bidhaa za machungwa nje ya nchi kuanzia Mwaka 2025.
(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma