Lugha Nyingine
Ukuaji wa uchumi wa Kenya wadorora kutokana na kupungua kwa shughuli katika baadhi ya sekta
Idara ya Takwimu ya Kenya (KNBS) imesema ukuaji wa uchumi wa Kenya umepungua hadi asilimia 5.3 katika robo ya kwanza ya mwaka huu, kutoka asilimia 6.2 katika kipindi kama hicho mwaka jana, ukiathiriwa na kupungua kwa shughuli za sekta za uzalishaji viwandani, ujenzi na uchukuzi.
KNBS imesema katika ripoti yake kuwa sekta ya kilimo ilikuwa na ukuaji mzuri na imesaidia kupunguza kasi ya kushuka kwa ukuaji wa uchumi. Ukuaji huo wa asilimia 5.3 umetokana kwa kiasi kikubwa na kuimarika kwa shughuli za kilimo, ambazo zilikua kwa asilimia 5.8, kutokana na mvua za kutosha zilizonyesha katika kipindi hicho.
Mwaka jana katika kipindi kama hicho sekta hiyo ilikua kwa asilimia 1.7 wakati Kenya ilipokuywa inasumbuliwa na ukame. Sekta nyingine zilizorekodi ukuaji katika robo ya kwanza ni pamoja na huduma za malazi na chakula (asilimia 21.5) TEHAMA (asilimia 8.7), fedha na bima (asilimia 5.8), na biashara ya kuuza bidhaa kwa jumla na rejareja (asilimia 5.7).
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma