久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

Magari kutoka China yapata umaarufu kwenye soko la magari la Angola

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 21, 2023

Picha hii iliyopigwa Juni 19, 2023 ikionyesha gari aina ya SUV la Kampuni ya Magari ya Geely, ambayo ni kampuni ya magari ya China, likiendeshwa kwenye barabara ya Luanda, mji mkuu wa Angola. Awamu ya Kwanza ya Maonyesho ya Magari ya Luanda ya Mwaka 2023 (Luanda Expo Car 2023) yamehitimishwa Jumapili baada ya kufanyika kwa siku tano huko Luanda, mji mkuu wa Angola. (Xinhua/Lyu Chengcheng)

Picha hii iliyopigwa Juni 19, 2023 ikionyesha gari aina ya SUV la Kampuni ya Magari ya Geely, ambayo ni kampuni ya magari ya China, likiendeshwa kwenye barabara ya Luanda, mji mkuu wa Angola. Awamu ya Kwanza ya Maonyesho ya Magari ya Luanda ya Mwaka 2023 (Luanda Expo Car 2023) yamehitimishwa Jumapili baada ya kufanyika kwa siku tano huko Luanda, mji mkuu wa Angola. (Xinhua/Lyu Chengcheng)

LUANDA - Awamu ya Kwanza ya Maonyesho ya Magari ya Luanda ya Mwaka 2023 (Luanda Expo Car 2023) yamehitimishwa Jumapili baada ya kufanyika kwa siku tano huko Luanda, mji mkuu wa Angola. Katika siku ya mwisho ya maonyesho hayo, mabanda ya kampuni za magari za China zilizoshiriki kwenye maonyesho hayo yaliendelea kuvutia watembeleaji wengi wa Angola.

Akiwa ameketi ndani ya modeli mpya iliyozinduliwa ya gari la UNI-K la Kampuni ya Magari ya Changan, kampuni ya kuunda magari yenye makao yake makuu mjini Jiangbei, Chongqing, Kusini-Magharibi mwa China, Alfredo Massango, mtembeleaji wa maonyesho hayo ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua, "Ni gari zuri. Linaonekana ni lenye kustarehesha sana na lenye nafasi kubwa ndani. Sasa, tunahitaji kujua kuhusu ufanisi wake, lakini mvuto wa kwanza ni chanya sana. Ninaamini yatapokelewa vyema nchini Angola."

Kwenye maonyesho haya ya magari, chapa za magari za China kama vile Changan, Jetour, Gac Motor, na Dongfeng zilichukua eneo kubwa la maonyesho. Eneo la maonyesho la chapa ya Changan lilikuwa kubwa zaidi kati ya chapa hizo za China, na uzinduzi wa modeli mbili mpya za magari katika soko la Angola pia ulitangazwa wakati wa maonyesho hayo ya siku tano yaliyofanyika kuanzia tarehe 14 hadi tarehe 18 Juni.

Moises Jonico, mkurugenzi wa mauzo na masoko wa Kampuni ya Magari ya Changan, amesema kuwa bidhaa za China zina uwezo mkubwa wa ushindani katika soko la Angola. Magari kutoka China yanathaminiwa kwa teknolojia, ufanisi, na kustarehesha, jambo ambalo huamsha shauku na upendeleo mkubwa miongoni mwa wanunuzi wa Angola.

"China imepiga hatua moja mbele kwenye masuala ya teknolojia na ufanisi katika modeli za magari yao. Kwenye soko letu, kila gari linalotumia teknolojia ya hali ya juu linaonekana kuwa jambo jipya. China imetuhimiza sisi wanunuzi wa Angola kuacha tabia ya kutumia magari ya kawaida na kutafuta teknolojia na ufanisi zaidi," amesema.

Pia ameliambia Xinhua kwamba magari yanayotumia nishati ya umeme ya China yana faida kubwa. Kwa sasa, magari mengi yanayoingizwa nchini Angola yanatumia nishati ya petroli. Bado, anaamini kwamba kama Angola itatoa uungaji mkono wa kisiasa kwa magari yanayotumia nishati ya umeme na kupanua miundombinu ya kuchaji, magari yanayotumia nishati mpya ya China pia yatafanya vyema nchini Angola.

"Teknolojia hii mpya kutoka kwa chapa za China, ambayo ni pamoja na magari yanayotumia nishati ya umeme na kutoa uchafuzi mdogo kwa mazingira, inawakilisha siku zijazo. Itanufaisha jamii na Dunia, kwa ajili ya wote watumiaji wa magari na wapenda magari nchini Angola," amesema.

Kampuni zaidi ya 80 kati ya kampuni zaidi ya 200 kwenye sekta ya magari katika soko la Angola zilishiriki kwenye maonyesho hayo ya magari. Kwa mujibu wa mratibu wa maonyesha hayo, watembeleaji zaidi ya 6,000 walishiriki.?

Picha hii iliyopigwa Juni 18, 2023 ikionyesha eneo la maonyesho la Kampuni ya Magari ya Jetour, ambayo ni kampuni ya magari kutoka China, kwenye Maonyesho ya Magari ya Luanda ya Mwaka 2023 (Luanda Expo Car 2023) huko Luanda, mji mkuu wa Angola. (Xinhua/Lyu Chengcheng)

Picha hii iliyopigwa Juni 18, 2023 ikionyesha eneo la maonyesho la Kampuni ya Magari ya Jetour, ambayo ni kampuni ya magari kutoka China, kwenye Maonyesho ya Magari ya Luanda ya Mwaka 2023 (Luanda Expo Car 2023) huko Luanda, mji mkuu wa Angola. (Xinhua/Lyu Chengcheng)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>