Lugha Nyingine
China kutarajia kuwa na soko la ndani la kufuata kanuni na sheria moja kuna manufaa kwa wawekezaji wa kigeni
Picha hii iliyopigwa kutoka angani Tarehe 23 Februari 2023 ikionyesha Bandari ya Qinzhou iliyo katika Mkoa unaojiendesha wa Guangxi, Kusini mwa China. (Xinhua)
BEIJING – Wizara ya Biashara ya China imesema Jumatatu kuwa, China inatarajia kuwa na soko la ndani la kufuata kanuni moja na sheria moja kutaleta mazingira bora na uwanja mkubwa zaidi kwa wadau mbalimbali wa soko, ikiwa ni pamoja na kampuni za biashara za ubia au zilizowekezwa na wafanyabiashara wa kigeni.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari, ofisa wa wizara hiyo Zhou Qiang amesema, "Soko la ndani tunalojenga la kufuata kanuni moja na sheria moja litakuwa soko la kiwango cha kimataifa na lililo wazi kabisa, na juhudi zaidi zitafanywa kutumia kikamilifu soko la ukubwa wa juu la China na kuhimiza kufungua mlango kwenye kiwango cha juu."
“Nchi italegeza zaidi ufikiaji wa soko kwa wawekezaji wa kigeni,” Zhou amesema, huku akiahidi kuwa hatua zinachukuliwa katika kufupisha ipasavyo orodha hasi ya China kwa uwekezaji wa kigeni na kuendana kwa kiwango cha juu na sheria na kanuni za kimataifa za uchumi na biashara ili kuimarisha mageuzi na kuhimiza mashirika ya kiuchumi kufunguliwa mlango kwa hatua madhubuti.
Zhou amesema, maonyesho ya uchumi, maonyesho ya biashara na mifumo maalum ya kikazi kwa miradi mikubwa ya uwekezaji wa kigeni itatumiwa ipasavyo kwa njia iliyoboreshwa ili kutoa majukwaa zaidi na huduma bora.
Amesema, juhudi pia zitafanywa kulinda vizuri zaidi maslahi halali ya wawekezaji wa kigeni, kujenga mazingira ya biashara ya soko huria, kufuata sheria na ya kimataifa.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma