Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping akutana na Waziri Mkuu wa Russia Mikhail Mishustin
Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Russia Mikhail Mishustin kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Mei 24, 2023. (Xinhua/Huang Jingwen)
BEIJING - Rais Xi Jinping wa China amekutana na Waziri Mkuu wa Russia Mikhail Mishustin Jumatano hapa Beijing.
Rais Xi amemwomba Mishustin kufikisha salamu zake za dhati kwa Rais Vladimir Putin wa Russia. Rais Xi amesema katika ziara yake ya kiserikali yenye mafanikio aliyoifanya Russia Mwezi Machi, yeye na Putin waliweka dira ya maendeleo ya baadaye kuhusu uhusiano na ushirikiano kati ya China na Russia katika nyanja mbalimbali.
“Ni matarajio ya watu na mwelekeo wa nyakati kuimarisha na kuendeleza uhusiano kati ya China na Russia,” Rais Xi amesema.
Amesema China na Russia zinapaswa kuendelea kuungana mkono kithabiti katika masuala yanayohusu maslahi yao ya msingi, na kuimarisha uratibu katika nyanja za kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa, Shirika la Ushirikiano la Shanghai, BRICS na G20.
“Pande hizi mbili zinapaswa kutumia fursa zaidi ili kuinua kiwango cha ushirikiano wa kiuchumi, biashara na uwekezaji, kuboresha taasisi na mifumo ya ushirikiano kati ya nchi mbili, kuimarisha na kupanua ushirikiano wa nishati na mawasiliano, na kutafuta maeneo mapya zaidi ya ukuaji wa uchumi,” Rais Xi amesema, huku akiongeza kuwa mabadilishano kati ya watu na kitamaduni yanapaswa kupanuliwa.
Rais Xi amesema China iko tayari kushirikiana na Russia na nchi wanachama wa Umoja wa Kiuchumi wa Ulaya na Asia ili kuunganisha Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja na Umoja wa Kiuchumi wa Ulaya na Asia ili kuwezesha uundaji wa soko kubwa la kikanda lililo wazi zaidi, kuhakikisha utulivu na urahisi wa minyororo ya kimataifa ya viwanda na ugavi, na kuleta manufaa yanayoonekana kwa nchi katika kanda hiyo.
Kwa upande wake Mishustin, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, ametoa salamu za dhati na za heri za Rais Putin kwa Xi. Amesema ziara ya Rais Xi nchini Russia Mwezi Machi ilikuwa yenye mafanikio makubwa, na imeanzisha zama mpya ya ushirikiano wa kiwenzi na kimkakati wa uratibu wa pande zote kati ya Russia na China.
Amesema Russia iko tayari kushirikiana na China ili kuhimiza kujenga Dunia yenye ncha nyingi na kuimarisha utaratibu wa kimataifa unaofuata sheria za kimataifa. Amesema, Russia inatarajia kuimarisha zaidi mabadilishano kati ya watu na ya kiutamaduni na China ili urafiki wa nchi hizo uweze kurithishwa kizazi hadi kizazi.?
Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Russia Mikhail Mishustin kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Mei 24, 2023. (Xinhua/Zhang Ling)
Habari Picha: Mandhari ya maeneo yanayozunguka Mto Bahe katika Mji wa Xi'an, China
Katika Picha: Watu wakivuna matunda ya bluberi katika Kijiji cha Wengbao, Mkoa wa Guizhou wa China
Habari Picha: Ndege wakionekana Lhasa, huko Tibet, Kusini Magharibi mwa China
Katika Picha: Tazama mandhari ya Mji wa Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma