Lugha Nyingine
Kampuni za kahawa za nje zinapoingia kwenye soko la China
Katika miaka ya hivi karibuni, kampuni nyingi zaidi za kahawa za nje zimeingia kwa wingi kwenye soko la China; wakati huo huo, kampuni za kahawa ambazo zimekuwa zikijikita nchini China kwa miaka mingi bado zinaonyesha nguvu ya uhai. Howard Schultz, mwanzilishi wa kampuni ya Kahawa ya Starbucks, alisema kwenye hotuba yake aliyoitoa katika Chuo Kikuu cha Peking hivi karibuni, "Idadi ya mikahawa ya Starbucks nchini China itazidi 10,000."
Imani hiyo ya Schultz inatokana kwa msingi wake wa uhalisia. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Starbucks, katika miaka kumi iliyopita, idadi ya mikahawa ya Starbucks katika China Bara imeongezeka kwa karibu mara 10. Mwaka 1999, Starbucks ilikuwa na mkahawa mmoja tu nchini China; kufikia mwaka jana, idadi hiyo imeongezeka na kufikia zaidi 6,000.
Katika miaka 24 tangu kuingia katika soko la China, Kampuni ya Kahawa ya Starbucks imeshuhudia mabadiliko ya dhana ya wateja wa China kuhusu kahawa na kufungua fursa mpya. Siyo Starbucks pekee, bali pia chapa nyingi zaidi za kahawa kutoka nje ya nchi zimepata shughuli zao mpya za ukuaji wa biashara nchini China.
Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, mkahawa wa COSTA Coffee ulioko Mtaa wa Watembea kwa miguu huko Nanjing umeimarika zaidi, na mauzo yake ya kila mwezi yamerudi katika kiwango cha kipindi kama hicho kabla ya janga la UVIKO-19 Mwaka 2019. Katika soko la kahawa iliyo tayari kwa kunywewa nyumbani, Costa imeshika nafasi ya pili.
Kampuni ya kahawa ya Vietinamu, Zhongyuan Legend ilifungua mkahawa wake wa kwanza huko Shanghai Septemba mwaka jana. Kwa chapa hii ya "kahawa ya taifa" ya Vietnam, China imekuwa moja ya soko kuu, na takriban vikombe milioni 800 vya kahawa viliuzwa Mwaka 2021.
McCafé, chapa ya kahawa inayotengenezwa kwa mikono inayomilikiwa na McDonald's, ilitangaza Septemba mwaka jana kuwa inatarajia kuongeza takriban mikahawa 1,000 mipya Mwaka 2023, ambayo mingi yake itapatikana katika miji ya daraja la tatu. Wakati huo huo, McCafé pia itazindua bidhaa mpya kuendana na ladha ya kahawa ya wateja wa China, ikitumaini kusaidia kufikia ukuaji wa juu.
Sababu ya kutokea kwa hali ya kampuni za nchi za nje kuongeza uwekezaji wao katika soko la China ni ukuaji wa haraka wa soko la kahawa la China katika miaka ya hivi karibuni. Kwa mujibu wa "Ripoti ya Utafiti kuhusu Tasnia ya Kahawa nchini China Mwaka 2022" iliyotolewa na iResearch, Mwaka 2021, ukubwa wa soko la kahawa la China utakuwa na thamani ya takriban yuan bilioni 87.6, ikiwa ni ongezeko la 38.9% ikilinganishwa na mwaka uliopita. Ripoti hiyo inakadiria kuwa ifikapo Mwaka 2024, thamani ya soko la kahawa la China inatarajiwa kufikia yuan bilioni 190.
Habari Picha: Mandhari ya maeneo yanayozunguka Mto Bahe katika Mji wa Xi'an, China
Katika Picha: Watu wakivuna matunda ya bluberi katika Kijiji cha Wengbao, Mkoa wa Guizhou wa China
Habari Picha: Ndege wakionekana Lhasa, huko Tibet, Kusini Magharibi mwa China
Katika Picha: Tazama mandhari ya Mji wa Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma