Lugha Nyingine
Orodha ya "miji mipya ya daraja la kwanza" katika shughuli za kahawa za China: Soko la kahawa la hali moto ya mauzo ya ndani na lenye nguvu katika biashara ya nje
Siku chache zilizopita, Kampuni ya Usafirishaji Mizigo ya Manbang ilitoa takwimu kuhusu orodha ya "miji mipya ya daraja la kwanza" katika shughuli za kahawa nchini China.
Mahitaji ya usafirishaji yaongezeka
Katika miaka ya hivi karibuni, shughuli za kahawa zimekuwa zikipata maendeleo yenye ustawi nchini China. Kwa mujibu wa takwimu za Manbang, Mwaka 2022, kiwango cha usafirishaji wa kahawa kilipata pilika nyingi mara mbili mnamo Oktoba na Desemba, na ongezeko la usafirishaji wa kahawa mnamo Desemba katika mwaka huo lilizidi 30%. Katika kipindi cha Mwezi Machi 2023, watu wa ofisi nyingi kwenye majengo mijini walianza tena kazi zao, hivyo usafirishaji wa kahawa haraka "ulianza kuongezeka".
Orodha ya "miji mipya ya daraja la kwanza" katika shughuli za kahawa
Takwimu zilizotolewa na Manbang zimeonesha kuwa, Mji wa Suzhou wa Mkoa wa Jiangsu, China umepokea karibu tani 90,000 za kahawa katika mwaka uliopita, na kuwa kinara kwenye orodha ya kupokea kahawa kwa miji ya China. Kwa sababu chapa nyingi zinazojulikana zimeanzisha vituo vyao vya kukaanga buni huko Suzhou, na wakati huo huo, matumizi mapya ya kuvuka maeneo mahsusi ya matumizi ya kahawa kama vile kunywa kahawa + kutazama maonesho ya mchezo wa Sanaa wa Opera ya Kunqu, kunywa kahawa + kutembelea duka la vitabu yameibuka hapa. Takwimu zisizokamilika zimeonesha kuwa, kwa sasa kuna mikahawa na vioski vya kahawa zaidi ya 1,600 katika maeneo ya mijini na vijijini ya Suzhou, yenye wafanyakazi husika zaidi ya 10,000.
Mshindi wa pili katika orodha hiyo ya miji, Mji wa Kunming, kama "jirani wa karibu" wa Pu'er, "Mji Mkuu wa Kahawa wa China", umekuwa kituo cha usafirishaji wa buni za kahawa za Yunnan. Kila mwaka, kahawa ya Pu'er inasafirishwa kwenye masoko ya ng'ambo kupitia Kunming.
Huko Chengdu, katika Mkoa wa Sichuan utamaduni wa baa ndogondogo umekuza hali ya matumizi ya "kahawa ya kila siku na divai ya usiku"; huko Guangzhou, kuongeza mchuzi wa kahawa kwenye chakula kama soseji ambazo zilipikwa kwa unga wa mchele kumewafanya watu kuona mchanganyiko wa kipekee wa uenyejishaji.
Kwa ujumla, miji ya daraja la kwanza bado ni sehemu kuu za usafirishaji wa kahawa nchini China.
Kahawa haihitajiki tena katika miji mikubwa ya China?
Pamoja na maendeleo ya uchumi wa China katika miaka ya hivi karibuni, watumiaji katika miji mingi ya daraja la pili na la tatu wamegundua hatua kwa hatua "uhuru wa kahawa". Takwimu zilizotolewa hadharani zimeonesha kuwa, idadi ya maduka ya kahawa katika miji ya daraja la tatu iliongezeka kwa kasi zaidi na kufikia 19% kutoka Mwaka 2021 hadi Mwaka 2022.
Kwa mtazamo wa njia za usafirishaji, njia ya usafirishaji kahawa ya Pu'er "Pu'er-Kunming" imeorodheshwa ya kwanza kati ya njia maarufu zaidi za usafirishaji wa kahawa, mara 14 zaidi ya njia ya pili.
Kila mtu anapenda Kahawa ya Yunnan
Yunnan inapatikana kwenye "eneo la dhahabu la kukua" kwa kahawa ya Arabica.
Oda za mizigo za Kampuni ya Manbang zinaonyesha kuwa oda ya mbali zaidi ya usafirishaji wa kahawa inachukua umbali wa zaidi ya kilomita 7,000 kutoka Pu'er, Yunnan hadi Kunyu, Xinjiang.
Habari Picha: Mandhari ya maeneo yanayozunguka Mto Bahe katika Mji wa Xi'an, China
Katika Picha: Watu wakivuna matunda ya bluberi katika Kijiji cha Wengbao, Mkoa wa Guizhou wa China
Habari Picha: Ndege wakionekana Lhasa, huko Tibet, Kusini Magharibi mwa China
Katika Picha: Tazama mandhari ya Mji wa Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma