Lugha Nyingine
Rais wa China akutana na viongozi wa nchi za Asia ya Kati
Rais wa China Xi Jinping jana mjini Xi’an kwa nyakati tofauti alikutana na viongozi wa nchi za Asia ya Kati wanaoshiriki kwenye Mkutano wa viongozi wakuu kati ya China na Nchi za Asia ya Kati na kufanya ziara nchini China.
Alipokutana na mwenzake wa Turkmenistan Serdar Berdymukhamedov, Rais Xi amesema China iko tayari kushirikiana na Turkmenistan kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kupata maendeleo mapya, ili kuwanufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili.
Katika mazungumzo kati yake na mwenzake wa Tajikistan Emomali Rahmon, Rais Xi amesema China iko tayari kushirikiana na Tajikistan kuinua kwa pande zote kiwango cha ushirikiano katika sekta mbalimbali, ili kuhimiza ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya pande hizo mbili ambayo ina urafiki wa kudumu, mshikamano na kunufaishana na kupata mafanikio kwa pamoja.
Akizungumza na mwenzake wa Kyrgyzstan Sadyr Japarov, Rais Xi amesema China iko tayari kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya ujirani na urafiki mwema na kunufaika kwa pamoja na ustawi, ili kuchangia ustawi wa maendeleo ya nchi hizo mbili.
Alipokutana na mwenzake wa Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev, Rais Xi amesema China iko tayari kushirikiana na Uzbekistan kukuza ushirikiano kwa pande zote, ili kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya pande hizo mbili.
Habari Picha: Mandhari ya maeneo yanayozunguka Mto Bahe katika Mji wa Xi'an, China
Katika Picha: Watu wakivuna matunda ya bluberi katika Kijiji cha Wengbao, Mkoa wa Guizhou wa China
Habari Picha: Ndege wakionekana Lhasa, huko Tibet, Kusini Magharibi mwa China
Katika Picha: Tazama mandhari ya Mji wa Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma