Lugha Nyingine
Kahawa yawa kitambulisho cha uchumi wazi wa Jiji la Shanghai ili kukumbatia Dunia
Kwenye Jiji la Shanghai la China, tasnia ya kahawa inaonesha uhai wa kudumu unaokua, na utamaduni wa kunywa kahawa umekuwa mtindo wa maisha ya jiji hilo.
Mkahawa mpya wa Chapa ya Starbucks ulifunguliwa kwenye Jengo la Libao la Shanghai mwezi wa Septemba, 2022. (Picha kwa hisani ya serikali ya eneo la Huangpu la Shanghai)
Simulizi ya Kahawa na Shanghai
Miaka 170 iliyopita, Mwaka 1853, mfamasia wa Uingereza J. lewellyn alileta Shanghai kahawa, na kuiuza kwenye famasi. Wakati huo watu wa Shanghai waliita kahawa hiyo “dawa ya kikohozi”.
Mwaka 1866, mkahawa wa kwanza wa Shanghai “Mkahawa wa Hongkou” ulifunguliwa. Ulikuwa mahsusi kwa ajili ya kuhudumia mabaharia. Mkahawa huo siyo tu ulitoa huduma ya kahawa bali pia bia za aina mbalimbali ziliuzwa.
Mwaka 1958 ulishuhudia kuzaliwa kwa chapa ya kwanza ya kahawa inayojulikana ya Shanghai, “Kahawa Shanghai”.
Mwezi wa Mei, 2000, Chapa ya Kahawa ya Starbucks ilifungua mkahawa wake wa kwanza kwenye Barabara ya kati ya Huaihai ya Shanghai; Miaka 22 baadaye, Shanghai imekuwa mji wa kwanza duniani ambao idadi ya mikahawa ya chapa ya Starbucks imezidi elfu moja.
Takwimu kutoka ripoti ya “Mtazamo wa Shanghai 2023” zinaonesha kuwa, hadi kufikia mwezi Aprili, 2023, Shanghai ilikuwa na mikahawa zaidi ya 8,000, ikichukua NO.1 duniani, ikiyazidi kwa mbali majiji kama vile New York, London, Tokyo n.k. Shanghai ina wastani wa mikahawa 1.3 katika kila eneo la ukubwa wa kilomita moja ya mraba, na mikahawa 3.16 katika kila watu 10,000.
Mkahawa wa Starbucks wa “Kaskazini Zaidi” huko Shanghai. (Picha/Wu Yue)
Kahawa yaleta matumizi katika manunuzi ya aina mpya
Chapa ya mkahawa ya "Bear Claw" ambayo hutumia wafanyakazi walemavu kama watoa huduma, na mkahawa wa kumbukumbu ulioanzishwa mahsusi kuwahudumia wazee wenye matatizo ya utambuzi......mikahawa ya Shanghai ni ya aina mbalimbali na jumuishi.
Mkahawa wa chapa ya "Bear Claw". Picha imetolewa na Shirikisho la Walemavu la Shanghai.
“Kunywa kahawa katika Jiji la Shanghai haina ladha inayofanana. Huu ni moyo wa uvumbuzi wa kahawa ya Shanghai” anasema Zhu Dajian, profesa na msimamizi wa wanafunzi wa shahada ya uzamivu katika Shule ya Uchumi na Usimamizi ya Chuo Kikuu cha Tongji cha China.
Kahawa yaunganisha Shanghai na Dunia
Mnamo mwaka 2016, kwenye kando ya Mto Huangpu Tamasha la kwanza la utamaduni wa kahawa la eneo la kifedha la Lujiazui lilileta Shanghai dhana ya tamasha la wazi la kahawa kwa mara ya kwanza. Katika majira ya mchipuko ya mwaka 2023, tamasha hilo lilifanyika kwa awamu ya saba, hivyo kuwa tamasha kubwa zaidi la kahawa na linalofanyika mara kwa mara zaidi katika matamasha ya aina hiyo nchini China. Chapa zinazoshiriki kwenye tamasha hilo zimeongezeka kutoka 24 hadi 213.
Tamasha la saba la Utamaduni wa Kahawa la eneo la kifedha la Lujiazui. (Picha imetolewa na upande wa Lujiazui, Shanghai)
“Limekuwa dirisha la kuunganisha kahawa ya China na Dunia kutoka tamasha la kahawa la Shanghai” alisema mwandaaji wa tamasha hilo.
Aina na chapa nyingi zaidi za kahawa zinaingia Shanghai kwa kupitia majukwaa mbalimbali, kama vile Maonyesho ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE), hivyo kulifanya Jiji la Shanghai liwe “Mji Mkuu wa Kahawa Duniani” kwa uhalisia.
Chapa mbalimbali za kahawa duniani zimefungua mikahawa yao ya kwanza Shanghai, huku chapa za Shanghai zikienda nchi nyingine kwa ajili ya kupanua soko. Kwa kutumia kahawa kama kitambulisho, Shanghai inakumbatia Dunia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma