Lugha Nyingine
Uingiaji wa Uwekezaji wa moja kwa moja wa Kigeni (FDI) nchini China waongezeka kwa asilimia 2.2 katika miezi minne ya kwanza
Picha hii ya angani iliyopigwa Tarehe 13 Machi 2023 ikionyesha kituo cha kontena cha Bandari ya Taicang, Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China. (Xinhua/Li Bo)
BEIJING - Uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDI) katika China Bara, kwa matumizi halisi, uliongezeka kwa asilimia 2.2 mwaka hadi mwaka na kufikia yuan bilioni 499.46 katika miezi minne ya kwanza ya mwaka, Wizara ya Biashara ya China imesema Jumatano.
Kwa vigezo vya dola za Marekani, FDI ulishuka kwa asilimia 3.3 mwaka hadi mwaka hadi dola bilioni 73.5 za Marekani.
Takwimu kutoka wizara hiyo zinaonyesha kuwa, sekta ya utengenezaji wa bidhaa ilishuhudia uingiaji wa FDI ukiongezeka kwa asilimia 4.1 mwaka hadi mwaka na kufikia yuan bilioni 130.05 katika miezi minne ya kwanza, huku ule wa tasnia ya teknolojia ya hali ya juu ukiongezeka kwa asilimia 12.8 katika kipindi hicho.
Hasa uwekezaji wa kigeni katika utengenezaji wa bidhaa za teknolojia ya hali ya juu uliongezeka kwa asilimia 37.1, huku katika sekta ya huduma za hali ya juu ukiongezeka kwa asilimia 6.
Katika kipindi cha Januari-Aprili, uwekezaji kutoka Ufaransa na Uingereza uliongezeka kwa asilimia 567.3 na asilimia 323.7 mwaka hadi mwaka, mtawalia. Uwekezaji za kigeni wa moja kwa moja kutoka Japani na Jamhuri ya Korea ulipanda kwa asilimia 68.1 na asilimia 30.7, mtawalia, mwaka hadi mwaka.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma