Lugha Nyingine
Kenya yazindua msimbo wa QR (QR Code) ili kuchochea malipo kwa njia ya kidijitali
(CRI Online) Mei 05, 2023
Benki Kuu ya Kenya (CBK) kwa kushirikiana na benki za biashara na kampuni zinazotoa huduma za malipo, imezindua msimbo wa QR (QR Code) ili kuongeza matumizi ya malipo kwa njia ya kidijitali.
Gavana wa Benki hiyo, Patrick Njoroge, amewaambia wanahabari jijini Nairobi kuwa, QR Code hiyo italeta manufaa kwa wafanyabiashara na wateja wao. Amesema msimbo huo una taarifa zitakazoweza kutoa njia mbadala kwa wateja kufanya malipo kwa njia ya kidijitali katika maeneo mbalimbali ya mauzo, ikiwa ni pamoja na katika maduka makubwa na madogo.
(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma