Lugha Nyingine
Teknolojia za kisasa zawezesha huduma za treni za mizigo za kati ya China na Ulaya kwenye Kituo cha Kimataifa cha Uchukuzi cha China-Kazakhstan
Treni ya mizigo inayotoa huduma kati ya China na Ulaya iliyojaa aloi za chuma kutoka Kazakhstan iliwasili katika Kituo cha Kimataifa cha Uchukuzi cha China-Kazakhstan katika Mji wa Lianyungang, Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China Aprili 26.
Ikiwa ni kituo cha kwanza kujengwa tangu Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja lilipotangazwa, kituo hicho cha uchukuzi wa bidhaa kimehakikisha ufanisi mzuri tangu kilipozinduliwa Julai 2014. Ufanisi huu hautenganishwi na eneo la utumaji bidhaa lenye akili bandia la kituo hicho, ambalo pia huitwa "ubongo" wa kituo.
Picha ikionyesha alama ya ardhini ya kituo cha mashariki cha Daraja Jipya la Ardhini la Ulaya-Asia kwenye Kituo cha Kimataifa wa Uchukuzi wa Bidhaa cha China-Kazakhstan katika Mji wa Lianyungang, Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China. (Picha kwa hisani ya Bandari ya Lianyungang)
Cheng Fei, msimamizi mkuu wa utumaji bidhaa wa kituo hicho, kwa kawaida hutumia mfumo wa teknolojia za akili bandia kutoa maagizo ya upakiaji bidhaa kwa madereva. Yeye na wenzake wameshuhudia maelfu ya treni za China-Ulaya kwenye kituo hicho.
Kutokana na maendeleo ya sera, usimamizi na teknolojia, aina mpya za huduma za treni za mizigo za China-Ulaya, kama vile usafirishaji wa makontena kwa njia za ardhini, angani na baharini na uidhinishaji jumuishi wa forodha, zimeibuka kwenye kituo hicho na kupunguza muda wa usafirishaji wa makontena ya kimataifa kutoka zaidi ya siku nne hadi chini ya siku, huku ikipunguza muda wa usafiri kwa nusu.
Hadi kufikia Machi 14, 2023, kituo hicho kilikuwa kimeshughulikia zaidi ya safari 5,000 za treni za mizigo za China-Ulaya.
Kutokana na huduma zake za usafiri wa nchi kavu, Bandari ya Lianyungang ilishughulikia makontena milioni 1.46 ya bidhaa zenye uzito wa jumla wa tani milioni 76.35 katika robo ya kwanza ya mwaka huu, ikiwa ni ongezeko la asilimia 9.8 na asilimia 15.5, mtawalia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma