Lugha Nyingine
Simulizi ya Zawadi za Kitaifa za Rais Xi Jinping: Mfano wa Meli ya “Liulinhai”
Picha iliyopigwa mwezi Septemba, 2015 ikionesha zawadi kwa Xi Jinping kutoka kampuni ya Microsoft ya Marekani, mfano wa meli ya mizigo ya “Liulinhai” uliochapishwa kwa teknolojia ya 3D. Picha/Hu Yang
Rais wa China Xi Jinping alipokutana na maofisa viongozi wa Marekani huko Seattle, Marekani tarehe 22 Septemba, 2015, alitoa simulizi moja: Zaidi ya miezi mitatu tu baada ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Marekani, meli ya mizigo ya China “Liulinhai” ilifika bandari ya Seattle, ikikomesha historia ya kutokuwa na mawasiliano ya usafiri wa meli kwenye bahari kwa miongo kadhaa kati ya China na Marekani.
Katika siku iliyofuata Xi Jinping alitembelea makao makuu ya kampuni ya Microsoft, ambapo alipokea zawadi ya mfano wa meli ya “Liulinhai” uliochapishwa kwa teknolojia ya 3D. Kwenye kibao cha mfano wa meli hiyo kuna maandishi ya “Liulinhai: Usafiri wake ulianzia Mwaka 1979, ukifungua safari mpya ya urafiki kati ya China na Marekani, na kuwanufaisha watu wa China na Marekani — zawadi kutoka Microsoft”.
Usafiri wa kwanza wa meli ya “Liulinhai” umekuwa alama ya China kufungua mlango kwa dunia. Katika wakati wa ziara yake hiyo, Xi Jinping alifanya mazungumzo na mikutano mingi na wadau mbalimbali wa Marekani. Alisisitiza kuwa “Mlango wa China uliofunguliwa kamwe hautafungwa”.
Rais Xi Jinping alipozungumza kupitia njia ya video na Rais wa Marekani Joe Biden mwezi wa Novemba, 2021, alitumia mfano wa meli kwa kumithilisha: “China na Marekani ni kama meli mbili kubwa zinazosafiri kwenye bahari kubwa, lazima kushika barabara usukani wa meli, ili meli hizo mbili kubwa za China na Marekani zisafiri pamoja wakati wa kukabiliwa na mawimbi na upepo bila kuyumba, kukwama, na zaidi kutogongana.”
Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Marekani Joe Biden wakizumgumzana kwa njia ya video asubuhi ya tarehe 16, Novemba, 2021. Picha/Yue yuewei
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma