Lugha Nyingine
China yaeleza matarajio ya kuimarika kwa mahitaji katika manunuzi
Watu wakinunua vitu kwenye supamaketi huko Nanjing, Mkoa wa Jiangsu, China, Aprili 11, 2023. (Picha na Su Yang/Xinhua) |
BEIJING - Maofisa na wachambuzi wamesema kuwa, ingawa bei za vitu vya matumizi zilipandishwa polepole nchini China tangu mwanzoni mwa mwaka huu, lakini hakuna haja ya kuwa na wasiwasi juu ya kushuka kwa bei nchini China, kwani uchumi wake uko kwenye njia ya kufufuka kwa hatua madhubuti chini ya sera za uhimizaji wa uchumi zilizowekwa.
Kiwango cha bei za vitu vya watumiaji wa China (CPI) kikiwa kiashiria muhimu cha kiwango cha mfumuko wa bei, kilipanda kwa asilimia 0.7 mwezi Machi kuliko kiwango kile cha mwezi Machi mwaka jana, na kilipanda kwa asilimia 2.1 na asilimia 1 mwezi Januari na wa Februari mwaka huu.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika wiki hii, Fu Linghui, Msemaji wa Idara Kuu ya Takwimu ya China, amesema upunguaji wa bei hauonekani wazi nchini China kwa sasa na hautaonekana katika kipindi kijacho.
"Kupungua kwa bei kunahusiana na kushuka kwa kasi kwa kiwango cha bei ya jumla, mara nyingi huambatana na hali ya kupunguzwa kwa utoaji wa fedha na kudidimia kwa uchumi," Fu amesema.
Fu ametaja wastani wa ongezeko la asilimia 1.3 la CPI na upanuzi thabiti wa asilimia 4.5 kwenye Pato la Taifa (GDP) katika robo ya kwanza ya mwaka huu, pamoja na ukuaji wa kasi wa asilimia 12.7 wa M2, ambacho ni kiashiria cha utoaji wa fedha ikiwa ni pamoja na fedha taslimu na akiba zote benkini zilizo katika mzunguko hadi mwishoni mwa mwezi Machi.
Zou Lan, ofisa wa Benki ya Umma ya China, amesema kuwa ukuaji wa haraka wa mikopo ya fedha na kushuka kwa bei kimsingi ni matokeo ya kucheleweshwa kwa wakati.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma