Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping ampongeza Diaz-Canel kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Cuba
BEIJING - Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Rais wa China Xi Jinping Alhamisi alituma ujumbe wa pongezi kwa Katibu wa Kwanza wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Cuba na Rais wa Cuba Miguel Diaz-Canel Bermudez kwa kuchaguliwa kwake tena kuwa Rais wa Cuba.
Katika ujumbe wake, Rais Xi amesema hivi sasa, uhusiano kati ya China na Cuba unaendelea kwenye kiwango cha juu na maendeleo mapya yakifanywa kwa uendelevu.
Rais Xi ameongeza kuwa ziara ya Rais Diaz-Canel nchini China Mwezi Novemba mwaka jana ilikuwa yenye mafanikio makubwa, ambapo yeye na Diaz-Canel walifikia makubaliano muhimu ya kuendelea kuimarisha kwa pande zote uhusiano maalum na wa kirafiki kati ya China na Cuba katika zama mpya.
Rais Xi amesema anatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Cuba, na yuko tayari kudumisha mawasiliano ya karibu na Rais Diaz-Canel na kuendelea kuimarisha miongozo ya kisiasa ya uhusiano kati ya pande hizo mbili na nchi hizo mbili katika juhudi za pamoja za kujenga jumuiya ya China na Cuba yenye mustakabali wa pamoja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma