Lugha Nyingine
Jumba la Makumbusho ya Historia ya Viwanda vya Usafiri wa Anga vya China lazinduliwa Beijing
Picha hii iliyopigwa Aprili 16, 2023 ikionyesha hafla ya uzinduzi wa Jumba la Makumbusho ya Historia ya Viwanda vya Usafiri wa Anga ya China hapa Beijing, China. (Xinhua)
BEIJING - Jumba la Makumbusho ya Historia ya Viwanda vya Usafiri wa Anga vya China limezinduliwa mjini Beijing siku ya Jumapili, na kuwa mahali pekee pa kutoa maonyesho ya kina ya historia ya miaka 110 ya usafiri wa anga wa China.
Likiwa limejengwa Eneo la Miyun la Beijing, jumba hilo la makumbusho limejengwa kwa pamoja na wadau watatu wakuu katika sekta ya anga ya China: Kampuni ya Kundi la Viwanda vya Usafiri wa Anga la China, Kampuni ya Injini za Vyombo vya Anga ya China na Kampuni ya Ndege za Kibiashara ya China.
Zaidi ya vitu mbalimbali 1,400 vinaonyeshwa katika jumba hilo la makumbusho, ambalo lina ukubwa wenye kuchukua eneo la mita za mraba 3,328 na lina eneo la maonyesho lenye ukubwa wa karibu mita za mraba 2,400.
Ndege halisi na ndege za mfano kumi zinaonyeshwa kwa nje kwenye jumba hilo.
Kutokana na juhudi zisizo na kikomo, China imekuza mfumo wa kisasa wa viwanda vya usafiri wa anga na kujenga utamaduni wake wa usafiri wa anga. Jumba hilo la makumbusho linaonyesha matukio makubwa, bidhaa, shughuli na takwimu za uwakilishi katika maendeleo ya viwanda vya usafiri wa anga vya China, ikionyesha shauku, utamaduni na kujitolea kwa sekta hiyo ya China na watu wake, kwa mujibu wa jumba hilo la makumbusho.
Jumba hilo la makumbusho litafunguliwa kwa umma kutembelea bila malipo, likitumika kama jumba la kumbukumbu lenye maudhui ya historia ya usafiri wa anga na msingi wa elimu maarufu ya sayansi ili kupokezana kwa juhudi kubwa na moyo wa sekta ya anga ya China.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma