Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping asisitiza kuimarisha mageuzi, kupanua ufunguaji mlango na kuendeleza maendeleo ya kisasa ya China
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitembelea bandari katika Mji wa Zhanjiang, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, Aprili 10, 2023. Rais Xi Jumatatu alikagua Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China. (Xinhua/Yan Yan)
GUANGZHOU - Rais Xi Jinping wa China amesisitiza umuhimu wa kubaki imara katika kuimarisha mageuzi ya pande zote na kupanua ufunguaji mlango wa kiwango cha juu, na kuutaka Mkoa wa Guangdong, ambao ni mfano wa mageuzi na kufungua mlango, kuchukua uongozi katika kuendeleza maendeleo ya kisasa ya China.
Rais Xi, ameyasema hayo wakati wa kukagua Mkoa wa Guangdong China kuanzia Jumatatu hadi Alhamisi.
Rais Xi amesema Guangdong ni mtangulizi na mfano wa mageuzi na kufungua mlango wa China, na mkoa huo umetoa mchango wenye umuhimu mkubwa na kubeba jukumu kubwa katika kufikia maendeleo ya kisasa ya China.
Ameutaka mkoa huo kuongoza katika kuimarisha mageuzi ya pande zote, kuhimiza ufunguaji mlango wa kiwango cha juu, kuimarisha uwezo wa China kujiamini na kuwa na nguvu katika sayansi na teknolojia, kufanya mfumo wake wa viwanda kuwa wa kisasa, na kuratibu maendeleo yenye uwiano kati ya maeneo ya mijini na vijijini na kati ya maeneo.
Katika ziara yake hiyo ya ukaguzi, Rais Xi pamoja na ukaguzi wa maendeleo mbalimbali ya mkoa huo, ikiwa ni pamoja na ustawi wa mazingira asilia na viumbe vya majini kama vile misitu ya mikoko, pia alifahamishwa kuhusu jitihada za Mkoa wa Guangdong za kuboresha muunganisho wa kikanda kupitia ujenzi wa miundombinu bora ya uchukuzi na kuoanisha maendeleo yake na yale ya Bandari Huria ya Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China.
Rais Xi amesema, Sera ya China ya mageuzi na ufunguaji mlango itabaki bila kubadilika kwa muda mrefu.
Amesema China iko tayari kushirikiana na nchi yoyote yenye nia ya kufanya ushirikiano wa kunufaishana ili kuendeleza ustawi wa pamoja na maendeleo ya uchumi wa Dunia.
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akifahamishwa kuhusu jitihada za kuendeleza uzalianaji, uhifadhi na ukuzaji wa viumbe vya majini kwenye kituo cha kilimo cha majini katika Mji wa Zhanjiang, wa Mkoa wa Guangdong, China, Aprili 10, 2023. (Xinhua/Ju Peng)
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akifahamishwa kuhusu juhudi za kuimarisha ulinzi wa misitu ya mikoko kwenye eneo la misitu ya mikoko katika Mji wa Zhanjiang Aprili. 10, 2023. (Xinhua/Ju Peng)
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akifahamishwa kuhusu jitihada za kuimarisha uunganishaji wa miundombinu ya uchukuzi na kuendeleza maendeleo shirikishi kati ya Mkoa wa Guangdong na mkoa jirani wa kisiwa wa Hainan katika bandari ya Mji wa Zhanjiang wa Mkoa wa Guangdong, Aprili 10, 2023. (Xinhua/Yan Yan)
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitembelea bandari katika Mji wa Zhanjiang wa Mkoa wa Guangdong Aprili 10, 2023. (Xinhua/Ju Peng)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma