Lugha Nyingine
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wafanyabiashara wa Italia asema Soko la China limejaa fursa
Gari kutoka Italia likionyeshwa kwenye Maonyesho ya Tatu ya Kimataifa ya Bidhaa za Matumizi ya China (CICPE) huko Haikou mkoani Hainan, China, Aprili 11, 2023. (Xinhua/Pu Xiaoxu)
HAIKOU - Paolo Bazzoni, Mwenyekiti wa Shirikisho la Wafanyabiashara wa Italia nchini China (CICC), amesema soko la China limejaa fursa na anatazamia kampuni za Italia kuingia zaidi katika soko la pili kwa ukubwa la wanunuzi wa bidhaa duniani.
Kampuni nyingi zaidi za Italia zitaingia soko la China ikiwa mazingira mazuri yataendelea kuwepo, Bazzoni amesema katika mahojiano maalum na Shirika la Habari la China, Xinhua kwenye Maonyesho ya Tatu ya Kimataifa ya Bidhaa za Matumizi ya China (CICPE) yanayoendelea huko Hainan.
Uhusiano wa China na Italia umeimarishwa kidhahiri katika miaka ya hivi karibuni. Takwimu zinaonyesha kuwa thamani ya biashara kati ya nchi hizo mbili ilifikia thamani ya dola za Marekani bilioni 77.9 Mwaka 2022, ikiwa ni ongezeko la asilimia 5.4 kutoka kiwango cha mwaka jana.
Bazzoni anaamini uchumi wa China unaimarika tena ukijitoa kutoka kwa athari za UVIKO, na ameonyesha yake imani juu ya matarajio yake. Amesema hali hiyo nzuri haitatokea mara moja, lakini dalili chanya zinajitokeza.
Hadi kufikia mwisho wa Mwaka 2022, shirikisho hilo lilikuwa na wanachama 868, ikiwa ni ongezeko la asilimia 98.6 kuliko Mwaka 2019, huku idadi ya ofisi zake kote China ikiongezeka hadi saba, kwa mujibu wa CICC.
Akielezea kufurahishwa na Maonyesho ya Tatu ya Kimataifa ya Bidhaa za Matumizi ya China (CICPE), ambayo ni maonyesho ya kwanza makubwa ya kimataifa baada ya China kuboresha hatua zake za kukabiliana na UVIKO, Bazzoni amesema yatakuwa maonyesho mazuri kwa chapa za bidhaa za Italia na kampuni za Italia, kwani vyombo vya habari na watumiaji katika manunuzi ya bidhaa wataangalia kwa uangalifu maonyesho hayo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma